9 Agosti 2015 - 21:34
Obama: Netanyahu apiliza kwa kuingilia masuala ya Marekani

Rais Baraka Obama amesema: hakuna kiongozi yeyote wa nchi za nje anaye ingilia mambo ya ndani ya serikali ya Marekani kama waziri mkuu wa utawala wa Israel, kwa kweli amechupa mipaka katika kuingilia masuala ya ndani ya serikali ya Marekani

Shirika la habari AhlulBayt (a.s) ABNA: shirika la habari la Israel limesambaza habari ya mahojiano ya Rais wa Marekani Baraka Obama na mwandishi wa habari Faridi Zakaria wa CNN aliposema: hali ya waziri mkuu wa Israel ya kuingilia maswala ya ndani ya serikali ya Marekani yamepita kiwango
Aidha amesema katika mahojiano hayo yalio sambazwa usiku wa Jumapili, amefafanua matatizo yaliopo baina ya Israel na utawala wa Marekani kuhusu makubaliano ya mpango wa nyukilia wa Iran, huku akisisitiza kuwa ni makosa makubwa kwa Benjamin Netanyahu kuyapinga makubaliano hayo.
Alipokuwa akijibu swali la mwandishi wa habari wa CNN kuwa je hakuna kiongozi wa nje anayeingilia mambo ya ndani ya serikali ya Marekani kama Netanyahu? Pia kwa jinsi unavyo fahamu ilishawahi kutokea suala hilo la kuingilia mambo ya ndani kwa kiongozi wa nchi za nje ya Marekani? Rais Baraka Obama akijaribu kutojibu swali hilo kwa wazi alisema kumwambia mwandishi wa Habari kuwa: Zakaria swali hilo unapaswa umuulize Benjamin Netanyahu.
Obama alipokuwa akisisitiza kuwa ana uwezo wa kuthibitisha madhara ya Netanyahu kwa kupinga kwake makubaliano ya mpango wa nyuklia wa Iran akisema: makubaliano haya ndio njia Bora makini itakayo tuthibitishia kuwa isiweze kutengeza silaha za nyuklia, ambayo pia ni makubaliano mazuri kwa utawala sMarekani hususan kwa serikali ya Israel.
Kwamujibu wa ripoti hii, Netanyahu mnamo mwezi Machi mwaka huu alipinga mazungumzo ya muafaka wa nyuklia wa Iran na nchi zenye nguvu duniani alipokuwa anahutubia bunge la Marekani na kuyazungumzia makubaliano yanayoweza kutokea baina ya Iran na kikundi cha 5+1 kitu ambachokuchukia kitendo hicho.
Baada ya kusainiwa kwa makubaliano hayo baina ya Iran na nchi hizo, sitofahamu imeendelea kuzidi baina ya utawala wa Israel na Marekani, hata hivi mwisho marekani imefikia hatua ya kusema haya: Serikali ya Israel ndio pekee inayopinga makubaliano ya nyuklia ya Iran.

Mwisho wa Habari/290