23 Septemba 2015 - 10:46
Papa Francis aanza ziara nchini Marekani

Kiongozi wa Kanisa Katoliki duniani Papa Francis amewasili nchini Marekani kuanza ziara ambamo pia atahudhuria kikao cha Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa mjini New York, na kuzungumza katika kikao cha Congress ya Marekani,

Shirika la habari la ABNA linaripoti kuwa: Kiongozi wa Kanisa Katoliki duniani Papa Francis amewasili nchini Marekani kuanza ziara ambamo pia atahudhuria kikao cha Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa mjini New York, na kuzungumza katika kikao cha Congress ya Marekani, ambacho kinajumuisha Baraza la Wawakilishi na Baraza la Seneti. Papa Francis mwenye umri wa miaka 78 alipokelewa na Rais wa Marekani Barack Obama na mkewe Michelle Obama katika uwanja wa ndege za kijeshi wa Andrews karibu na Washington DC. Makamu wa Rais Joe Biden pia alikuwepo kumpokea Papa Francis, ambaye alisafiri kutoka Cuba katika ndege ya kampuni ya Alitalia. Katika ziara yake ya siku tatu nchini Cuba, Papa Francis aliwataka raia wa nchi hiyo kuyazingatia mapinduzi mapya ya upendo na huruma. Amewataka pia wacuba kujenga daraja na kupandikiza mbegu za maridhiano, wakati ambapo juhudi zinaendelea kurejesha uhusiano kati ya nchi hiyo na Marekani.

Mwisho wa habari/ 291