27 Oktoba 2015 - 22:38
Magaidi wa Daesh 21 waangamizwa magharibi mwa Iraq

Makao makuu ya habari za kijeshi nchini Iraq imesambaza habari ya kuuwawa kwa magaidi 21 wa kikundi cha kigaidi cha Daesh katika mashambulio yaliofanywa na majeshi ya Iraq magharibi mwa nchi hiyo

Shirika la habari AhlulBayt (a.s) ABNA: makao makuu ya habari za kijeshi nchini Iraq ambayo yako chini ya wizara ya ulinzi nchini humo siku ya Jumanne imetangaza kuwa: majeshi ya Iraq  yamefanikiwa kufanya mashambulizi makali katika sehemu kadhaa muhimu za vikundi vya kigaidi vya Daesh magharibi mwa nchi hiyo.
Aidha katika kufafanua ujumbe huo wameeleza kuwa kambi ya kijeshi ya Al Jazirah na Al Badiyah katika mashambulio yake ya kusafisha maeneo yanayokaliwa na magaidi wa Daesh mashariki mwa mkoa wa Baghdad iliopo katika mkoa wa Al Anbar ambapo wamefanikiwa kuikomboa sehemu hiyo baada ya kuwaangamiza magaidi wa Daesh 21 katika eneo hiyo.
Kwamujibu wa ripoti ya shirika la habari la Sputnik limetangaza kuwa: makao makuu ya habari za kijeshi nchini Iraq yametangaza kuwa majeshi ya nchi hiyo yaliopo katika barabara ya mji mpya inayokwenda mjini Baghdadi imekombolewa kutoka mikononi mwa magaidi wa Daesh.
Majeshi ya Iraq pia yamekomboa hospitali iliokuwa katika upande wa mashariki mwa Baghdad kutoka mikononi mwa magaidi wa Daesh.   
mwisho wa Habari/290