Shirika la habari AhlulBayt (a.s) ABNA, ikinukuu kutoka shirika la habari la Irna: shirika la habari la lugha ya kikurdi (Rudaw) limenunukuu kutoka kwa mwakilishi wa kikundi cha Democratic cha Kurdistan nakutanga kuwa: watoto 12 waliokuwa wakifanya juhudi za kutoroka katika kambi ya mafunzo ya kijeshi ya kikundi hicho cha Kigaidi cha (Assalam) kiliopo katika mkoa wa Mosul, ama baada ya kufahamu magaidi hao walikamatwa na kunyongwa.
Video nyingi zimesambazwa na kikundi hicho cha kigaidi zikionyesha jinsi gani watoto wakipewa mafunzo ya kuuwa, yakiwa ni maandalizi kwaajili ya kufanya mashambulio ya kigaidi dhidi ya wananchi wasiokuwa na hatia nchini humo.
Aidha siku kumi ziliopita kamanda aliokuwa amejisalimisha kutoka katika kikundi hicho cha kigaidi amesema: kikundi hicho cha kigaidi miezi mitatu iliopita wameyonga watu 200 wa kikundi hicho ambao ni wananchi kutoka Chechnya, ambao wameuliwa kwa makosa kama hayo.
mwisho wa Habari/290