Kwa mujibu wa Shirika la Habari la Kimataifa la Ahlul-Bayt (as) –ABNA– Jiji jipya la makombora la Kikosi cha Anga na Anga za Juu cha Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu (IRGC) limezinduliwa rasmi, katika hafla iliyohudhuriwa na Meja Jenerali Ali Abdollahi, Mkuu wa Majeshi ya Iran, pamoja na Meja Jenerali Seyyed Majid Mousavi, Kamanda wa Kikosi cha Anga na Anga za Juu cha IRGC.
Katika uzinduzi huo, aina mbalimbali za makombora ya balistiki na makombora ya kusafiri (cruise missiles), pamoja na mifumo yake ya kurushia, zimeoneshwa.
Aidha, Meja Jenerali Abdollahi, sambamba na kufichua jambo hilo jipya lililoelezwa kuwa la kushangaza, alikagua mafanikio ya hivi karibuni na kiwango cha utayari wa kivita wa Kikosi cha Anga na Anga za Juu cha IRGC.









Maoni yako