21 Novemba 2015 - 18:42
Majeshi ya Iraq waikomboa sehemu ya (zaituni) katika mkoa wa Al Anbar

Majeshi ya Iraq katika mwendelezo wa mashambulio yake ya kuyakomboa maeneo yanayokaliwa na vikundi vya kigaidi vya Daesh, leo katika wilaya ya Ramadi wamefanikiwa kulikomboa eneo la Zaituni katika mkoa wa Al Anbar nchini humo.

Shirirka la habari AhlulBayt (a.s) ABNA: vyanzo vya Iraq siku ya Jumamosi vimetanga kuikomboa sehemu ya Zaituni katika wilaya ya Ramadi katika mkoa wa Al Anbar kutoka mikononi mwa vikundi vya kigaidi nchini humo.
Televisheni ya Alalam akithibitisha habari hiyo imesisitiza kuwa majeshi ya kupambana na magaidi nchini humo wamefanikiwa kuikomboa sehemu ya Zaituni iliopo kusini mwa mje wa (Alhamsah Kilo) ambapo katika mashambulio hayo makumi ya magaidi wa Daesh wameangamia katika mashambulizi hayo na kuikomboa sehemu hiyo.
Eneo la (Ahamsah Kilo) liko katika mkoa wa Al Anbar ambapo siku ziliopita mkoa huo ulikombolewa na majeshi ya Iraq yakishirikiana na Nguvu za kijamii, huku wakiendeleza kufanya mashambulizi hayo kwa lengo la kuyakomboa maeneo yaliobaki katika mkoa huo.
mwisho wa Habari/290