23 Novemba 2015 - 16:43
Rais mteule wa Argentina Mauricio Macri aahidi mageuzi katika sekta ya uchumi

Rais mteule wa Argentina Mauricio Macri aahidi mageuzi katika sekta ya uchumi

Shirika la habari la ABNA linaripoti kuwa: Rais mteule wa Argentina Mauricio Macris ameahidi kufufua uchumi wa taifa hilo ambao umekuwa ukiporomoka kwa kufanya mageuzi katika nyanja mbalimbali za kiuchumi na kuboresha mfumo wa soko huru la biashara .

Ushindi wa bwana Mauricio Macris umehitimisha utawala wa Rais Cristina Fernandez pamoja na marehemu mume wake katika kipindi cha zaidi ya muongo mmoja uliokuwa umegubikwa na migogoro.

Hata hivyo wakati Rais huyo mteule akiingia madarakani rasmi mnamo Dec. 10, mwaka huu ataanza majukumu yake huku akikabiliwa na changamoto ya mfumuko wa bei ya kwa kiwango cha asilimia 30 na matumizi makubwa ndani ya serikali huku pia akikosa idadi kubwa ya wabunge ya kumuwezesha kupitisha marekebisho atakayopendelea yafanyike.

" Macri ataanza majukumu yake katika mazingira magumu sana ya kisiasa, atakumbana na wakati mgumu katika kufanya maboresho katika nyanja za kiuchumi" anasema Daniel Kerner ambaye ni mshauri wa masuala ya kiuchumi.

Katika asilimia 98 ya kura zilizokwishahesabiwa tayari, katika uchaguzi huo uliofanyika siku ya jumapili, Macris alikuwa kashinda kwa asilimia 51.5 ukilinganisha na asilimia 48.5 ya mgombea wa chama tawala Daniel Scioli,ambaye tayari amekubali kushindwa katika uchaguzi huo.

Ushindi huu unakomesha kipindi cha hali mbaya ya kisiasa na kiuchumi nchini humo ikiwa ni pamoja na mahusiano hafifu yaliyokuwepo ya kidiplomasia miongoni mwa mataifa kadhaa ikiwemo Marekani.

"Leo ni siku ya kihistoria, na ni kipindi cha mabadiliko sasa" alisikika bwana Macri huku akishangiliwa na wafuasi wake.

Wakati wa kipindi cha kampeni Bwana Macri aliahidi kuwa msikivu na mtendaji zaidi tofauti na ilivyokuwa wakati wa utawala wa Fernandez.

Aahidi kutolipiza kisasi

Akihutubia maelfu ya wafuasi wake siku ya jumapili, Bwana Macri alisema hatalipiza kisasi katika kipindi cha utawala wake bali atajikita katika mipango ya maendeleo ya taifa hilo.

" Najisikia mwenye furaha sana kwa sababu leo ndio tumehitimisha utawala wa kimafia" alisikika akisema Felisa Sanchez ambaye ni mfuasi wa Bwana Macri huku akipeperusha bendera ya taifa hilo.

Macri ambaye sasa ametimiza umri wa miaka 56 ameahidi pia kuvutia wawekezaji ikiwa ni pamoja na kupunguza viwango vya kodi zisizo za lazima katika maeneo kadhaa.

Hata hivyo anatarajiwa kupata upinzani mkubwa bungeni wakati atakapochukua hatua za maboresho hayo ya kiuchumi.

Rais huyo anatokea katika moja ya familia zenye utajiri mkubwa nchini humo na umaarufu wake aliupata zaidi kupitia katika masuala ya kandanda wakati alipokuwa Rais wa kilabu moja maarufu ya Boca Junior nchini humo.

Mwisho wa habari / 291

 

Siku tatu za maombelezi Mali

Shirika la habari la ABNA linaripoti kuwa: Mali leo(23.11.2015) imeanza siku tatu za maombolezi ya kitaifa kuwakumbuka wahanga wa mashambulizi ya kigaidi yaliyofanyika kutokana na kuzingirwa hoteli ya kifarahari, yaliyowaua watu 19 kwenye mji mkuu, Bamako.

Mataifa mengine ya jirani kama Senegal, Mauritania na Guinea zinaungana na taifa hilo kuonyesha mshikamano.

Uchunguzi wa kuwasaka waliohusika na mkasa huo bado unaendelea ambapo mpaka sasa hakuna utambuzi wa idadi wala utaifa wa wanaotuhumiwa kufanya shambulizi hilo ambalo limegharimu maisha ya watu 19, ambalo vilevile makundi mawili ya jihadi yamekiri kuhusika nalo.

Siku ya umwagikaji damu

Katika mkasa huo uliotokea Ijumaa watu waliokuwa na silaha waliizingira hoteli ya ya kifahari ya Radisson Blu, na kuwateka wafanyakazi na wageni wa hoteli 170. Shambulizi hilo lilifikia kikomo baada ya jeshi la Mali na vikosi vya kimataifa walishambulia jengo hilo, ambapo watu 19 waliuwawa, wakiwemo raia wa kigeni 14.

Waliouwawa katika mkasa huo ni pamoja na Warusi sita, Wachina watatu, Wabelgiji wawili, Mmarekani mmoja, Muisrael mmoja, Msenegali na idadi nyingine ya wanajeshi wa Mali.

Rais ya Senegal atoa pole

Rais wa Senegal, Macky Sall, jana Jumapili alitembelea mji wa Bamako kuonyesha mshikamano kwa Mali, mwanachama wa Jumuiya ya Uchumi ya nchi za Afrika Magharibi-ECOWAS, ambayo kiongozi huyo ni mwenyekiti. Sall alisema Mali haitakuwa mpweke katika mapambano hayo, kwa sababu wote wanahusika.

Katika hatua nyingine jana Jumapili, wachunguzi nchini Mali inafuatilia kwa kina vyanzo mbalimbali vya uchunguzi wao kufuatia mauwaji hayo. Siku mbili baada ya mkasa huo ambao makundi ya Al Mourabitoun na al-Qaeda katika katika eneo la Afrika Magharibi yamedai kuhusika, kumekuwa na utambuzi duni wa waliofanya shambulizi.

Katika taarifa yake kitengo cha usalama wa taifa nchini Mali kimenukuliwa na katika televisheni ya nchi hiyo kikisema maeneo kadhaa yamekuwa yakifuatiliwa. Na kwamba hoteli iliyokuwa imeshambuliwa imekuwa ikifuatiliwa kwa uangalifu mkubwa.

Kwa kuzingatia siku ya operesheni ya kukabiliana na ugaidi katika hoteli hiyo Rais Ibrahim Bouba Keita alisema wote kwa pamoja wauwaji walifanikiwa kuuwawa katika eneo la hotel ingawa kulikuwa na taarifa nyingine za awali zilizosema kulikuwepo na mshambuliaji mwengine.

Ufaransa, ambalo lilikuwa lilikuwa likiitawala Mali katika enzi za ukoloni, linasaidia katika jitihada za sasa za uchunguzi na kwamba imetuma timu ya wataalamu katika kufanikisha jambo hilo.

Umwagikaji damu mjini Bamako ni miongoni mwa ishara za hivi karibuni kabisa kw kuzorota zaidi kwa hali ya usalama katika taifa hilo la Afrika Magharibi. Wanamgambo wenye itikadi kali wenye kuungana na al-Qaeda walilidhibiti eneo la jangwa la kaskazini 2012 lakini mwaka mmoja baadae walitawanywa na operesheni ya kijeshi ya Ufaransa.

Mwisho wa habari / 291