Shirika la habari AhlulBayt (a.s) ABNA: ikinukuu kutoka katika televisheni ya Almayadin kuwa imetoa taarifa inayohusu barua ya serikali ya Ankara kuitaka serikali ya Moscow kukutana na kufanya mazongumo.
Televisheni hiyo imetangaza kuwa: ikulu ya Kremlin katika ujumbe wake imetangaza kuwa Rais wa Uturuki ametoa rasmi ombi la kutaka kuonana na Rais wa Urusi siku ya Jumatatu katika kikao kinachofanyika mjini Paris Ufaransa.
Hii ni katika hali ambayo vyombo vya habari vya kimataifa vimesambaza habari inayohusu kupiga simu kwa Rais wa Uturuki kwa Rais wa Urusi ambapo Rais wa Urusi hakuwa mwenye kuijibu simu ya Rais mwenzake.
Waziri wa mambo ya nje wa Urusi muda punda baada ya kusambaa habari ya simu ya Rais wa Uturuki kwa Rais wa Urusi, amethibitisha habari ya simu hiyo kuwa Rais wa Urusi hakuwa mwenye kuipokea simu ya Rais wa Uturuki.
mwisho wa Habari/290