Shirika la habari AhlulBayt (a.s) ABNA: majeshi ya Syria yamepata ushindi mwingine katika mkoa wa Halab ambapo wamefanikiwa kukikomboa kijiji cha Tamureh kilichopo Humeh ya Kaskazini katika mkoa wa Halab.
Kijii hicho kiko upande wa kusini mwa magharibi mwa miji ya Nabil na Zahra ambapo ni moja kati ya sehemu walizokuwa wakitumia vikundi vya kigaidi vya Daesh katika kurusha Roketi na makomora kuelekea mikoa wanaishi wafuasi wa madhehebu ya shia nchini humo.
Majeshi ya Syria kwa kufanikiwa kwake kwa kukikomboa kijiji cha Tamureh wamemiliki nguzo kubwa ya kulinda maeneo ya pembeni mwa miji ya Nabil na Zahra kwa umbali wa kilometa tatu kwenda mji wa Andani ambapo ndio makao maalumu ya ngome ya vikundi vya kigaidi katika eneo la Humeh ya kaskazini katika mkoa wa Halab.
Majeshi ya Syria pia yamefanikiwa kukikomboa kijiji cha Jalbul Kalb sehemu ya Humeh ya mashariki mwa mkoa wa Halab kutokana na vikundi vya kigaidi vya Daesh.
Majeshi ya Syria baada ya kuitoa miji ya Nabil na Zahra katika kuzingirwa na magaidi wa Daesh siku hadi siku wameonekana wakisonga mbele katika maeneo ya Humeh ya kaskazini na Humeh ya mashariki mwa mkoa wa Halab na kuwaondoa magaidi hao.
mwisho wa habari/290