Shirika la habari la ABNA linaripoti kuwa: Majeshi ya serikali ya Uturuki yamewashambulia wapiganaji wa vikosi vya kikurdi wanaoungwa mkono na Marekani kaskazini mwa Syria kwa siku mbili mfululizo licha ya Marekani kutoa mwito wa kuitaka Uturuki kusimamisha hatua yake hiyo. Shirika linalofuatilia haki za binadamu nchini Syria lenye makao yake Uingereza limesema kwamba wanajeshi wa Uturuki wameshambulia ngome zinazoshikiliwa na vikosi vya jeshi linaloongozwa na wakurdi DFS muungano ambao unafungamanishwa na kundi lenye nguvu la wakurdi YPG katika eneo la kaskazini na kaskazini magharibi mwa mkoa wa Aleppo. Kiasi wapiganaji wawili wa DFS wameuwawa na wengine saba wamejeruhiwa katika kipindi cha masaa 24 yaliyopita. Uturuki jana iliapa kuendeleza mashambulizi hayo na kuvitaka vikosi hivyo vya wakurdi kuondoka kwenye maeneo hayo.
Marekani na Uturuki zimekuwa zikilitumia kundi la kigaidi la Daesh kwa malengo binafsi ambapo Uturuki ilikuwa unalitumia kundi hilo kupigana na wakurdi na Marekani imekuwa ikilitumia kundi hilo kupigana na serikali halali ya Syria.
Marekani na Uturuki zimejikuta zikikosana kuhusu kushambuliwa wakurdi ambao si magaidi licha ya kuwa nchi hizo mbili zimekuwa zikitumia makundi ya kigaidi kufikia malengo yao.
Uturuki na Saudia arabia pia zimepanga kupeleka vikosi vyao vya ardhini nchini Syria ili kuyasaidia makundi ya kigaidi kupambana dhidi ya serikali ya Syria.
Serikali ya Uturuki ambayo imekuwa ikituma magaidi nchini Syria na kudhani kuwa serikali ya Syria itaanguka, inajikuta katika hali ngumu baada ya majeshi ya Syria kusonga mbele na kuyashinda makundi ya kigaidi, Uturuki inahofu hatima yake ikiwa serikali ya Syria itaendelea kutawala.
Mwisho wa habari/ 291