Shirika la habari la ABNA linaripoti kuwa: Rais Barack Obama wa Marekani leo hii amewataka raia wa taifa lake kutowanyanyapaa Waislamu kufuatia mashambulizi yanayofanywa na waislamu wa dhehebu la Sunni wahabia ambao wanadhaminiwa na Saudia arabia , yaliosababisha mauwaji ya mjini Brussels, akisema kwa kufanya hivyo ni sawa na kwenda kinyume na vita dhidi ya itikadi kali. Katika taarifa yake ya kila wiki kwa vyombo vya habari Obama amesema Wamarekani Waislamu ni washirika muhimu katika mapambano ya kitaifa dhidi wale wanaotaka kuendesha vita vya jihadi. Obama ameyasema hayo wakati ulimwengu ukiendelea kuwa kwenye mfadhaiko, kufuatia mashambulizi ya Jumanne nchini Ubelgiji, yanayodaiwa kufanya na kundi la kigaidi la Daesh, ambayo yalisababisha vifo vya watu 31, wakiwemo Wamarekani na watu wengine 300 kujeruhiwa.
Marekani na Saudia arabia zimekuwa zikiyasaidia makundi ya kigaidi nchini Syria ili kuiangusha serikali ya Syria, magaidi hao wameanza kurudi nchini mwao baada ya kushindwa vita dhidi ya serikali ya Syria na hivyo wanaendeleza mashambulizi katika nchi mbalimbali.
Mwisho wa habari/ 291