Shirika la habari la habari la ABNA linaripoti kuwa: serikali ya Israel ambayo ni mshirika wa karibu wa Uturuki imetoa onyo jipya la usafiri kwa raia wake kuelekea Uturuki. Nchi hiyo imewataka raia wake kuondoka nchini Uturuki haraka iwezekanavyo na kujiepusha kusafiri kwenda katika taifa hilo. Kitisho hicho kilichoelezwa kuwa cha uhakika wa hali ya juu ndiyo onyo la kiwango cha pili kwa ukubwa ambalo Israel inaweza kutoa. Aidha kitisho hicho kimeongeza maelekezo yaliyotolewa baada ya kuuwawa watalii watatu wakisraeli katika mashambulizi ya kujitoa mhanga mjini Istanbul mapema mwezi Machi. Baraza la usalama wa taifa la Israeli limetahadharisha hii leo kwamba kitisho cha kutokea mashambulizi mengine zaidi ya makundi ya kigaidi kinaongezeka na hasa mashambulio ya kundi la kigaidi la Daesh dhidi ya maeneo ya watalii na kwa ujumla kwa watalii wa kiisraeli. Kadhalika nchi hiyo imetoa tahadhari kama hiyo kwa raia wake katika nchi za Tunisia, Afghanistan na Pakistan. Pia imetoa tahadhari ya juu kwa eneo la rasi ya Sinai, Somalia, Sudan na Libya.
Israel ni moja kati ya nchi zinazolisaidia kundi la kigaidi la Daesh ili kuiangusha serikali ya Syria.
Mwisho wa habari/ 291