12 Aprili 2016 - 15:13
Saudia Arabia na Uturuki kujadili hali ya Syria + Picha

Viongozi wa serikali mbili za Saudia arabia na Uturuki ambazo zimekuwa zikiyasaidia waziwazi makundi ya kigaidi nchini Syria ili kuiangusha serikali ya Bashar asad wanakutana kujadili mabadiliko yanayowakabili kutokana na kushindwa vita kila siku...

Shirika la habari ABNA linaripoti kuwa: Viongozi wa serikali mbili za Saudia arabia na Uturuki ambazo zimekuwa zikiyasaidia waziwazi makundi ya kigaidi nchini Syria ili kuiangusha serikali ya Bashar asad wanakutana kujadili mabadiliko yanayowakabili kutokana na kushindwa vita kila siku.

Mfalme Salman wa Saudi Arabia yuko nchini Uturuki kuhudhuria mkutano wa kila mwaka wa shirika la ushirikiano la nchi za kiislamu OIC . Mfalme Salman anatarajiwa kufanya mazungumzo na Rais wa Uturuki Recep Tayyip Erdogan

Mfalme wa Saudi Arabia,Salman Bin Abdel- Aziz, aliwasili mjini Ankara jana kuanza ziara nchini Uturuki yenye lengo la kuimarisha uhusiano ambao tayari ni wa ndani baina ya nchi yake na Uturuki.

Mfalme Salman tayari amekutana na mwenyeji wake, Rais Erdogan na kuzungumzia juu ya mgororo wa nchini Syria na juu ya kile wanachokidai kwenye vyombo vya habri kuwa ni kupambana na magaidi Daesh ambao nchi hizo mbili zinawasaidia silaha na mahitaji mengine.

Mfalme wa Saudia awashangaza wengi baada ya kukodi hotel nzima

Vyombo vya habari nchini Uturuki vimeripoti kuwa mtawala huyo wa Saudi Arabia amefikia kwenye hoteli yenye ukubwa wa mita za mraba 4,850 mjini Ankara. Hoteli hiyo ina madirisha yenye vihami dhidi ya risasi na milango iliyojengwa kwa saruji inayoweza kuzuia mabomu. Inaripotikuwa kuwa kabla ya kuingia kwenye hotel hiyo aliamuru kila kitu kibadilishwe na kuwekwa vitu vipya kwa ajili ya ziara yake ya siku chache tu.

Mfalme wa Saudi Arabia aliwasili nchini Uturuki kutokea Misri. Ujumbe wa watu mia tatu ulitangulia mjini Ankara kuratibisha mambo ya malazi,itifaki na usalama wa mfalme.

Saudi Arabia na Uturuki zimeujenga tena uhusiano wa ndani baina yao baada ya uhusiano huo kuharibika kutokana na njama za Saudi Arabia katika kuondolewa madarakani kwa aliekuwa Rais wa Misri Mohammed Mursi wa Misri mnamo mwaka wa 2013. Mursi alikuwa mshirika mkubwa wa Uturuki.

Uturuki na Saudi Arabia zimekuwa zinashirikiana katika vita vya nchini Syria dhidi ya Rais Bashar-al Assad. Katika vita hivyo nchi hizo mbili zimekuwa zinawaunga mkono magaidi wanaowania kumwondoa madarakani Rais Assad, zikishirikiana na Marekani, Israel, Umoja wa Ulaya na baadhi ya nchi za kiarabu ambazo ni washirika wa Saudia arabia.

Mnamo mwezi wa Februari ndege za kijeshi za Saudi Arabia ziliwasili kwenye kituo cha Incirlik kusini mwa Uturuki ili kushiriki katika kile walichokidai kuwa ni kuwashambulia magaidi wa Daesh nchini Syria, lakini ndege hizo zimekuwa zikiwashushia misaada ya silaha , vyakula na madawa magaidi hao ili waweze kupambana na vikosi vya serikali ya Syria.

Hapo Alhamisi,Mfalme wa Saudi Arabia Salman, ataanza kushiriki kwenye mkutano wa kilele wa shirika la ushirikiano la nchi 57 za kiislamu, OIC. Wajumbe kwenye mkutano huo wa siku mbili watalijadili suala la Wapalestina, migogoro baina ya nchi wanachama na njia za kupambana na ugaidi .

Mkutano huo wa 13 utafanyika katika muktadha wa migogoro katika nchi kadhaa za Kiislamu, ikiwa pamoja na Yemen na Syria. Wakuu wa serikali na viongozi wa nchi zaidi ya 30 wanatarajiwa kushiriki kwenye mkutano huo chini ya uenyekiti wa Rais wa Uturuki Erdogan.

Maafisa wa shirika la ushirikiano la nchi za Kiislamu wameipitisha ajenda ya mkutano na watafuatiwa na mkutano wa matayarisho wa mawaziri wa mambo ya nje hapo kesho na Jumatano. Wakuu wa serikali na viongozi wa nchi watakutana kwa siku mbili kuanzia Alhamisi.

Wakati huo huo Rais Tayyip Erdogan amemtunukia Mfalme Salman medali ya heshima ya juu kabisa ya nchini Uturuki. Rais Erdogan ameeleza kuwa mtawala huyo wa Saudi Arabia amevishwa medali hiyo ya heshima kama ishara ya kuutambua mchango mkubwa alioutoa katika kuendeleza uhusiano wa kirafiki baina ya nchi yake na Uturuki.

Saudi Arabia imeibuka kuwa mshirika mmojawapo muhimu wa Uturuki baada ya kipindi cha mvutano. Mnamo mwaka huu majeshi ya nchi hizo yalifanya mazoezi ya kijeshi ya pamoja na zimekuwa zinajenga mshikamano thabiti wa kijeshi.

Saudia arabia ambayo hapo zamani ilikuwa inaheshima ya kuwa nchi tulivu kwa sasa inapoteza heshima hiyo kutokana na matukio ya kinyama inayoyafanya ikiwemo kuwasaidia magaidi wa Daesh na makundi mengine ya kigaidi yanayoua watu hovyo nchini Syria na Iraq, pia kutokana na nchi hiyo kuvamia nchi ya Yemen na kufanya mashambulizi hatari yaliyopelekea vifo vya zaidi ya watu 7000 wasio na hatia.

Mwisho wa habari/ 291