16 Aprili 2016 - 14:14
 Kiongozi wa Umoja wa Ulaya awasili Iran

Mwanadiplomasia wa ngazi ya juu kabisa wa Umoja wa Ulaya Federica Mogherini amewasili leo hii mjini Tehran, Iran

Shirika la habari la ABNA linaripoti kuwa: Mwanadiplomasia wa ngazi ya juu kabisa wa Umoja wa Ulaya Federica Mogherini  amewasili leo hii mjini Tehran, Iran, ikiwa ni ziara yake ya kwanza kabisa tangu makubaliano ya nyuklia kati ya Iran yaridhiwe wakati huu kukiwa na mvutano wa namna ya utekelezaji wake.  Mogherini, ambae alikuwa akiongoza mazungumzo kwa upande wa mataifa sita yalio katika makubaliano hayo, ameandamana na maafisa wengine wa juu wa Umoja wa Ulaya. Amepangiwa kukutana na waziri wa mambo ya nje wa Iran Javad Zarif. Ziara yake hiyo ya siku moja inafanyika baada ya Iran kuonesha wasiwasi kuhusu vikwazo vya kibenki, ambapo maafisa wanasema mataifa ya Magharibi, na hasa Marekani, bado inaweka vikwazo kwa Irani kuingia katika wa mfumo wa kifedha wa ulimwengu.

Iran na Umoja wa Ulaya na Marekani zinatofautiana katika mambo mengi ikiwemo suala la Syria ambapo Umoja wa Ulaya na Marekani zinaunga mkono waasi na kuwapa misaada ya silaha ili kuendeleza vita nchini Syria kwa lengo la kuiangusha serikali ya Bashar assad kama walivyofanya Libya, ambapo Iran inapinga kabisa vita hivyo vilivyosababisha maelfu ya watu kuuawa na wengine kukosa makazi.

Mwisho wa habari/ 291