6 Mei 2016 - 20:06
Bendera ya Iran zapepea katika barabara za Iraq + picha

Baadhi ya wananchi wa wilaya ya Basra nchini Iraq wamesambaza bendera ya Iran pamoja na picha za kamanda Qasim Suleimani katika barabara za wilaya hiyo.

Shirika la habari AhlulBayt (a.s) ABNA: wananchi wa Iraq wametoa jibu la vitendo kwa vikundi vilio dhidi ya Serikali ya jamhuri ya kiislamu ya Iran nchini humo baada ya wafuasi wa kikundi cha Baathi kuivunjia heshima serikali ya jamhuri ya kiislamu ya Iran.
Idadi kubwa ya wananchi wa wilaya ya Basra nchini Iraq waliamua kupeperusha bendera ya Iran katika barabara za mji huo, huku wakisambaza picha za kamanda wa jeshi la Quds Haji Qasim Suleimani.
Wananchi hao walipoulizwa sababu ya hatua yao hiyo walisema kuwa: wamefanya hilo kwaajili ya kuishukuru serikali ya jamhuri ya kiislamu ya Iran kwa misaada yake katika kupambana na kikundi cha kigaidi cha Daesh nchini humo.
Siku kadhaa zilisopita baadhi ya wafuasi wa kikundi cha Baath ambao walijitokeza na kuchanganyika na waandamanaji nchini humo yaliofanyika nchini humo, huku wakitoa kauli mbiu inayoashiria kuwa dhidi ya serikali ya kiislamu ya Iran, kitu ambacho kimepingwa vikali na viongozi, vyama vya kisiasa na wananchi wa Iraq.
Wabunge wa chama cha (Al Ahrar) ambacho kiko chini ya fikra ya Sadriyah wametangaza kuwa (Mugtada Sadri) kiongozi wa kikundi hicho amepinga vikali kauli mbiu dhidi ya Iran ziliotolewa katika maandamano yaliofanyka mjini Baghdadi Iraq.