Shirika la habari AhlulBayt (a.s) ABNA: kwa mujibu wa madai ya vyombo vya habari vya kikurdi, Abubakar Al-Bagdadiy” kiongozi wa kikundi hicho cha kigaidi amewataka watu wake nchini Iraq kujiandaa haraka iwezekanavyo kwaajili ya kuondoka nchini humo kwenda sehemu nyingine.
Kiongozi wa bunge la kiislamu la kislamu nchini Iraq pia ameashiria kumfikia barua waliopata wapiganaji wa Iraq iliokuwa na Muhuri wa Abubakar Al-Baghdadiy ambapo katika mambo muhimu yalioandikwa katika barua hiyo ni suala lilioashiriwa hapo juu.
“Ammar Hakim” akithibitisha suala hilo kupitia barua hiyo amesema: Abubakar Al-Baghdadiy amewataka wafuasi wake kuanza kujikusanya kwaajili ya kuondoka katika maeneo yaliokuwa chini yao na kuziacha sehemu hizo na kwenda sehemu zingine.
Aidha ameitaka serikali ya Iraq kufanya haraka kutoa ratiba ya kuzikomboa sehemu zinazokaliwa na magaidi hao, kwani maeneo hayo yanahtajia kujengwa tena upya kwa sababu katika muda ambao magaidi wa Daesh wanapokuwa katika miji hiyo uharibu maeneo hayo.
Mwana siasa huyo wa Iraq amemalizia kwa kusisitiza kuwa: hivi sasa ndio mwanzoni mwa kukisambaratisha kikundi cha Daesh nchini Iraq na kinapaswa kisambaratishwe haraka iwezekanavyo nchini humo.
“Wahidi Bakuziy” mmoja katika ya viongozi wa chama cha Wakurdi wa Iraq “Democratic Party” amesema kuwa naye ameipata barua hiyo inayowataka magaidi hao kuliacha taifa la Iraq na kutafuta pahala pengine, akibainisha hilo amesema: kilichopo katika barua hiyo ni amri ya Abubakar Al-Baghdadiy kwa makamanda wake nchini Iraq kwamba waanze kujianda kutoka katika mikoa ya Iraq, kwani wananchi wa Iraq na Syria hawana hadhi ya kutumikiwa na utawala wa kikundi hicho cha kigaidi.
Naye ameashiria suala lingine ambalo limeashiwiwa katika barua hiyo kuwa kiongozi wa Daesh amewataka magaidi wa Daesh kuiangalia kwa makini nchi ya Libya na mkoa wa Misrata, na kuto zitilia umuhimu sehemu walizo miliki katika nchi ya Iraq na Syria.
Katika wiki za hivi karibuni katika vita vya Syria na Iraq kumefanywa mashambulizi makali kupitia wapiganaji wa kislamu katika maeneo muhimo za kikundi hicho katika nchi hizo.
Nchini Iraq wapiganaji wa kujitolea wakishirkiana na majeshi ya taifa hilo na majeshi maalumu wamejikusanya katika mashambulizi ya kuikomboa Fallujah ambayo ni mji wa pili kwa ukubwa uliochini ya Daesh, na sasa mji huo umesha zingirwa na wapiganaji wa Iraq.
Nchini Syria pia wapiganaji wa nchi hiyo wakisaidiwa na majeshi umoja wa kupambana na magaidi uliokuwa chini ya Marekani yamefanya mashambulii makali katika mji wa Raqqa ambayo ndio makao makuu ya kikundi hicho cha kigaidi nchini humo, na kwamujibu wa ripote za mwisho kuhusu mji huo ni kwamba majeshi ya Syria yamefanikiwa kuingia katika mji huo.
mwisho wa Habari/290