Shirika la habari AhlulByt (a.s) ABNA: “Mahathir Mohamad” waziri mkuu aliyepita wa serikali ya Malaysia ameyasema hayo katika mahojiano yaliokuwa na mada ya “ harakati za kupambana na Ushia” ambapo amesema; suala la kupambana na Ushia nchini Malaysia hawaliafiki wananchi wote wa Malaysia, kwani baadhi ya wananchi hawapendi uwepo wa mashia nchini Malaysia na wananchi wengine hawana msimamo wowote kuhusu suala hilo.
Aidha ameongeza kusema kuwa: asilimia miamoja ya kabila la Malayu ni wafuasi wa madhehebu ya Sunni, hivyo kama itapatikana madhehebu nyingine nchini Malaysia itakuwa ni sababu ya kutokea tofauti na khitilafu ndani ya Taifa na ndio maana hatutaki madhehebu nyingine nchini Malaysia kwakuwa tija yake ni magomvi na malumbano.
“Mahathir Mohamad” aliendeleza kusema kuwa: tatizo ni hili kwamba nchini Malaysia hairuhusiwi dini na madhehebu yeyote nyingine kuwepo katika kabila la Kimalayu. Wewe kama mmalayu huna haki kujiunga na dini yinyngine yeyote wala hupaswi kwenda dhehebu lingine kwani kufanya hivyo ni kinyume na kanuni yetu. Kamwe huwezi kumuona mmalayu nchini Malaysia ana dini ya Kibuddha au dini ya Kihindu na kuhusu madhehebu ya Shia ndivyo hivyohivyo. Mashia wanaruhusiwa kuja na kuishi nchini Malaysia ama hawaruhusiwi kusambaza dhehebu lao na kuingilia masuala ya madhehebu yetu na kufanya juhudi ya kushawishi mmalaysia kujiunga na madhehebu ya Shia.
Waziri huyo wa zamani ambaye kwa sasa ni katibu mkuu wa taasisi ya amani ulimwenguni “Pradana” mwaka uliopita alisema kuwa: kuenea kwa mafunzo ya dhehebu la Shia katika jamii ya waislamu wa Malaysia, kutapelekea marumbano, khitilafu katika jamii hiyo, kitu ambacho kitaifanya jamii hiyo kusambaratika.
“Mahathir Mohamad” amesema: waislamu wa Malaysia watabaki katika saada na amani endapo wananchi wake wote watahakikisha kuwa wanafuata mafunzo ya madhehebu ya Sunni, huku akisisitiza kuwa katika baadhi ya jamii zilioingia na mafunzo ya kishia sasa zimekuwa na khofu na kutahayari katika jamii yao.
mwisho wa Habari/290