30 Julai 2016 - 15:28
Ujerumani yaituhumu Urusi kwa ukatili nchini Syria

Waziri wa mambo ya nje wa Ujerumani Frank-Walter Steinmeier ambaye nchi yake inaunga mkono upande wa waasi nchini Syria ameishutumu Urusi kwa janga la kibinaadamu lililojitokeza katika mji wa Aleppo nchini Syria.

Shirika la habari la ABNA linaripoti kuwa: Waziri wa mambo ya nje wa Ujerumani Frank-Walter Steinmeier ambaye nchi yake inaunga mkono upande wa waasi nchini Syria ameishutumu Urusi kwa janga la kibinaadamu lililojitokeza katika mji wa Aleppo nchini Syria.

Takribani raia  250,000 wamezingirwa wakati majeshi ya serikali ya Syria yanayoungwa mkono na Urusi yakiendelea na mashambulizi ya mabomu katika mji huo. Sasa Urusi imetangaza operesheni kubwa ya kuwafungulia njia ya kuwawezesha wananchi kukimbia wakiwa chini ya usalama na magaidi wanaoungwa mkono na Ujerumani na washirika wake kujisalimisha.  Lakini jumuiya ya kimataifa inahofu kuwa hatua ya Urusi ni mbinu tu ya ujanja wa serikali kuwatimua na kuwakamata magaidi wanaoungwa mkono na Marekani na washirika wake wa Ulaya na Uarabuni. Umoja wa Mataifa umeitolea wito Urusi kukabidhi udhibiti wa njia hizo  za kanda zenye usalama kwa mashirika ya misaada ya kibinadamu.

Kuvunjwa kwa ngome hiyo ya magaidi kutapelekea kushindwa kwa magaidi hao wanaodhaminiwa na Marekani na washirika wake, jambo lilipelekea nchi hizo kutumia vyombo vya habari kuharibu hatua hizo za kijeshi za Urusi dhidi ya magaidi hao hatari.

Mwisho wa habari/ 291