Shirika la habari la ABNA linaripoti kuwa: Mahakama moja ya mji wa kaskazini mwa China wa Tianjin imemhukumu kifungo cha miaka saba na nusu jela mwanaharakati mmoja kwa tuhuma za kuhujumu madaraka ya nchi. Huyo ni mwanaharakati wa pili kushtakiwa na kuhukumiwa kufuatia hatua ya kukamatwa mamia ya wanasheria wa haki za binadamu pamoja na wanaharakati nchini humo. Hu Shegin ambaye aliwahi kushiriki katika vuguvugu la kuunga mkono demokrasia pamoja na kuendesha kwa siri shughuli za makanisa ya kikristo kadhalika amepokonywa haki yake ya kisiasa kwa miaka mitano kwa mujibu wa mahakama hiyo. Taarifa ya mahakama imesema kwamba mwanaharakati huyo mwenye umri wa miaka 61 ametumia taasisi yake ya kidini kupata uungaji mkono wa mawakili wasiokuwa halali na kuwalipa makundi ya watu kusambaza fikra na mitizamo ya kuhujumu madaraka ya nchi na chuki dhidi ya serikali.
Mwisho wa habari/ 291