Shirika la habari AhlulBayt (a.s) ABNA: “Abdulazizi bin Abdillah Ali Sheikh” ambaye ndiye Mufti mkuu wa Saudi Arabia katika mazungumzo yake amewataka wawekezaji, wenye mashirika binafsi na Bank mbalimbali nchini humo kutengeza mfuko maalumu wa kuwasaidia wanajeshi wa Saudi Arabia waliopo katika vita ya Yemen.
Aidha Mufti huyo wa Saudi Arabia ameyasema hayo katika hali ambayo nchi hiyo katika mwaka mmoja uliopita walipunguza bajeti ya nchi hiyo kutokana na bei ya mafuta kushuka, kupunguzwa kwa bajeti ya mwaka kwa taifa hilo, kumepelekea hali ya maisha ya wananchi wa taifa hilo kuwa mbaya, na kusababisha wananchi wa nchi hiyo kutoridhika.
Toka mwaka mmoja wa Uvamizi wa Saudi Arabia nchini Yemen, mamia ya wanajeshi wa Saudi Arabia wameangamia katika mapigano yanayoendelea nchini humo na wanajeshi wa Yemen.
Majeshi ya Yemen katika wiki kadhaa ziliopita katika mwendelezo wa kujibu mashambulizi ya majeshi ya Saudi Arabia, wameongeza mashambulizi katika kambi za wanajeshi wa Saudi Arabia kusini mwa Saudi Arabia.
mwisho wa Habari/290