Shirika la Habari la ABNA linaripoti kuwa: Serikali ya Uturuki imeikosoa Ujerumani, ikisema madai ya Ujerumani kwamba Uturuki imekuwa kiota cha makundi ya kigaidi, yanaonyesha upungufu wa akili.
Wiki hii, kituo cha utangazaji cha serikali hapa Ujerumani, ARD, kilichapisha sehemu ya waraka wa siri wa serikali ambapo imetolewa tathmini kwamba Rais Recep Tayyip Erdogan na serikali ya Uturuki zinaunga mkono Waislamu wenye itikadi kali na makundi ya ugaidi. Katika tamko lake, serikali ya Uturuki imeyaita madai hayo kuwa jaribio la kuilenga Uturuki na kumlenga pia Rais wake. Aidha, Uturuki imeiomba Ujerumani ifafanue kauli zilizoko kwenye waraka huo wa siri. Uhusiano kati ya Uturuki na nchi za Magharibi umekuwa tete, tangu lilipofanyika jaribio la kuipindua serikali mwezi mmoja uliopita.
Nchi za Ulaya na Uturuki zimekuwa zikishirikiana kuwasaidia magaidi nchini Syria ili waangushe serikali ya Bashar asad, lakini baada ya jaribio lililofeli la mapinduzi dhidi ya serikali ya Uturuki , kumekuwa na sintofahamu kati ya Uturuki na washirika wake wa Ulaya na Marekani, kwani Uturuki inahisi bayana kuwa nchi hizo zilikuwa na mkono katika mapinduzi hayo.
Mwisho wa habari/ 291