Shirika la habari la Ahlubayt (as)ABNA: Richard Black seneta wa zamani wa chama cha Republican katika jimbo la Virginia amesema hayo leo Jumapili wakati alipohojiwa na shirika la habari la Associated Press na huku akiashiria siasa za kiuadui za serikali ya Donald Trump dhidi ya sheria za kimataifa na mikataba iliyokuwa imewekwa baina ya Marekani na nchi nyingine amesema, anaamini kwamba, Joe Biden, rais mteule wa Marekani atafuata siasa za mambo ya nje ambazo zitakuwa na mikwaruzano michache na nchi nyingine.
Vile vile amesema, anaamini kwamba, Biden hatokuwa na mielekeo ya kuingilia siasa za kigeni za nchi za Ulaya na nchi nyingine ambazo bado ni wanachama wa makubaliano ya kimataifa ya nyuklia maarufu kwa jina la JCPOA. Nchi hizo ni Jamhuri ya Kiislamu ya Iran, Russia, China, Uingereza, Ufaransa, Ujerumani pamoja na Umoja wa Ulaya.
Seneta Richard Black pia amesema, huenda siasa zitakazochukuliwa na Joe Biden kuhusu Iran zitapingwa na chama cha Republican hivyo anatarajiwa kwenda pole pole na kuchukua misimamo kwa tahadhari kuhusu Iran ili kuepusha mikwaruzano ya ndani.
Mwezi Mei 2018, Donald Trump aliitoa kijeuri Marekani katika makubaliano ya kimataifa ya nyuklia JCPOA na kuirejeshea Iran vikwazo vyote ilivyokuwa imeondolewa baada ya makubaliano hayo. Bali alikuwa akijigamba kwamba ameiwekea Iran vikwazo vya kiwango cha juu kabisa ambavyo haijawahi kuwekea nchi yoyote ile duniani. Hata hivyo taifa la Iran limefelisha vikwazo hivyo kwa muqawama wake wa kiwango cha juu kabisa.
342/