Shirika la habari la Ahlubayt (as)ABNA: Fawzi Barhoum, msemaji wa Harakati ya Muqawama wa Kiislamu ya Palestina HAMAS amesisitiza kuwa, utawala dhalimu wa Israel unafuta visingizio kwa ajili ya kudumisha mzingiro na mashambulio yake dhidi ya Ukanda wa Gaza.
Kiongozi huyo mwandamizi wa Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Palestina HAMAS amesema, hii kwamba, daima Israel imekuwa ikiionyeshea kidole cha lawama harakati hiyo na kuitaja kuwa ndio inayobeba dhima ya matukio ya Gaza, ni utafutaji visingizio tu vya kudumisha mzingiro na mashambulio ya jeshi lake dhidi ya eneo hilo ambalo ni nembo halisi ya muqwama na kusimama kidete.
Utawala wa Kizayuni wa Israel unalizingira eneo la Ukanda wa Gaza tangu mwaka 2006 wakati Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Palestina (HAMAS) ilipoibuka na ushindi katika uchaguzi wa Bunge la Palestina.
342/