25 Septemba 2026 - 21:50
Programu ya Asubuhi ya Kimaanawi Yaendelea katika Madrasat Hazrat Zainab (sa), Kigamboni

Wanafunzi wa Madrasat Hazrat Zainab (sa), Kigamboni, Dar es Salaam, wameendelea na programu ya kila siku ya asubuhi kwa kusoma Qur’ani Tukufu, dua na ziyara mbalimbali, kwa lengo la kuimarisha malezi ya kiroho, maadili ya Kiislamu na uhusiano wao na Qur’ani pamoja na Ahlul-Bayt (as).

Kwa mujibu wa Shirika la Habari la Kimataifa la Ahlul-Bayt (as) – ABNA–  Wanafunzi wa Madrasat Hazrat Zainab (sa), Kigamboni, Dar es Salaam, wameendelea na programu ya asubuhi ya kimaanawi inayohusisha usomaji wa Qur’ani Tukufu, dua na ziyara mbalimbali, kwa lengo la kuanza siku ya masomo kwa kumkumbuka Mwenyezi Mungu na kuimarisha uhusiano wao na Qur’ani pamoja na mafundisho ya Ahlul-Bayt (as).

Programu hii imefanyika tarehe 23 Septemba 2026 katika Madrasat Hazrat Zainab (sa), iliyopo Kigamboni, Dar es Salaam, kwa kushirikisha wanafunzi wa shule hiyo.

Programu hiyo hufanyika kila siku kwa mwendelezo, ambapo wanafunzi huanza siku yao ya masomo kwa kusoma Qur’ani Tukufu, dua na ziyara mbalimbali, jambo linalowasaidia kuanza shughuli zao za kielimu wakiwa katika mazingira ya kumkumbuka Mwenyezi Mungu na kuzingatia mafundisho ya dini.

Miongoni mwa ziyara zinazosomeka katika programu hiyo ni Ziyara Amina-Allah, Ziyara Warith, Ziyara Aal Yasin na Ziyara Ashura.

Kuendelea kwa programu hii ya kiroho kunalenga kuimarisha malezi ya kidini na kimaadili ya wanafunzi, kuwajengea mazoea ya kumkumbuka Mwenyezi Mungu, kuimarisha uhusiano wao na Qur’ani Tukufu na Ahlul-Bayt (as), pamoja na kukuza maadili mema katika maisha yao ya kila siku.

Aidha, programu hiyo huchangia kujenga mazingira ya shule yanayojikita katika malezi ya kiroho, elimu na maadili ya Kiislamu, sambamba na kuwaandaa wanafunzi kuwa na mwenendo mwema na misingi imara ya kidini.

Imeandaliwa na: Kitengo cha Mahusiano ya Umma – Uwakilishi wa Jamiat Al-Mustafa (s) Tanzania

Lebo

Maoni yako

You are replying to: .
captcha