Shirika la habari la Ahlubayt (as)ABNA: Rais wa Uturuki alisema hayo jana baada ya kuondoka katika Msikiti wa Hagia Sophia mjini Istanbul alikoswali Swala ya Ijumaa na kueleza kwamba, Emmanuel Macron ni msiba kwa nchi ya Ufaransa.
Rais huyo wa Uturuki amesema pia kuwa, hivi sasa nchi ya Ufaransa inapitia kipindi hatari mno kutokana na kuweko madarakani mtu kama Emmanuel Macron.
Hii si mara ya kwanza kwa Rais wa Uturuki kumshambulia kwa maneno Rais Emmanuel Macron wa Ufaransa.
Majuma kadhaa yaliyopita Rais Recep Tayyip Erdoğan wa Uturuki alinukuliwa akisema kuwa, Rais wa Ufaransa, Emanuel Macron, anahitaji kupimwa uwezo wake wa kiakili baada ya matamshi ya kibaguzi aliyotoa karibuni kuhusu dini ya Uislamu.
Aidha Erdogan alisema kuwa, Ufaransa itafanya uchaguzi wa rais yapata mwaka mmoja ujao ambao utaainisha hatima ya Macron, na kwamba anaamini huo utakuwa mwisho wake kwa sababu hajaifanyia lolote Ufaransa seuze nafsi yake mwenyewe.
Mwezi Septemba mwaka huu pia rais huyo wa Uturuki alinukuliwa akisema kuwa, historia ya Afrika ni historia ya Ufaransa pia na Wafaransa waliua raia milioni moja wa Algeria na watu laki 8 nchini Rwanda; kwa msingi huo hawawezi kutoa somo la ubinadamu kwa taifa la Uturuki ambalo halijawaua Waafrika.
342/