Shirika la habari la Ahlubayt (as)ABNA: Rais Hassan Rouhani amesema hayo leo katika kikao cha Baraza la Mawaziri la serikali yake na huku akisisitiza kwamba, kama Marekani itetekeleza ahadi zake zote, bila ya shaka yoyote Iran nayo itatekeleza ahadi zake zote amesema, taifa la Iran linaendelea na njia yake kwa nguvu zake zote na wakati wowote upande wa pili unapoheshimu sheria, basi Iran inaipokea kwa furaha hatua hiyo.
Rais Rouhani ameashiria pia ushindi wa kila aina lilioupata taifa la Iran katika vipindi vitatu muhimu vya historia na kuvitaja vipindi hivyo kuwa ni vya mwamko wa Mapinduzi ya Kiislamu, vita vya kulazimishwa na vita vya kiuchumi vilivyoanzishwa na maadui dhidi ya Iran na kusisitiza kuwa, mtu yeyote duniani hapaswi kudhani kwamba anaweza kulipigisha magoti taifa la Iran kwa vikwazo na vita vya kiuchumi.
Katika sehemu nyingine ya hotuba yake, Rais wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amezungumzia pia kuanguka ndege ya Ukraine tarehe 8 Januari 2020 karibu na Tehran na huku akiwapa pole tena wafiwa amesema, uadilifu utatendeka kuhusu ajali hiyo.
Tarehe 8 Januari 2020 ndege moja ya abiria ya Ukraine ilianguka karibu na Tehran na kupelekea watu 167 kupoteza maisha wakiwemo wahudumu 9 wa ndege hiyo.
Wengi wa abiria hao walikuwa raia wa Iran, na abiria 32 walikuwa na pasi za kusafiria za nchi tano za Canada, Afghanistan, Ukraine, Uingereza na Uswisi.
342/