2 Juni 2025 - 20:21
Source: Parstoday
Hamas: Jinai za Israel Gaza zinashinda uhalifu wa Wanazi

Afisa mwandamizi wa Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Palestina Hamas amelaani shambulizi la karibuni la Israel dhidi ya wananchi wa Kipalestina wenye njaa waliouawa shahidi wakiendea chakula cha msaada kusini mwa Gaza, akibainisha kwamba mauaji haya yanatuma ujumbe wa wazi kwa ulimwengu wa Kiislamu kwamba wakati umefika wa kusimama dhidi ya wauaji.

Sami Abu Zuhri amelaani shambulio hilo baya la Israel dhidi ya waombaji misaada wa Gaza, akilieleza kuwa ni baya zaidi kuliko uhalifu wa kifashisti na Manazi wa Ujerumani, huku akiutaka ulimwengu wa Kiislamu kukabiliana na watenda jinai hao.

Mapema jana, Ofisi ya Vyombo vya Habari vya Serikali ya Gaza iliripoti kuwa wanajeshi wa Israel waliwafyatulia risasi raia wa Kipalestina karibu na kituo cha msaada huko Rafah na kuua watu wasiopungua 30 huku wengine wengi wakijeruhiwa.

Abu Zuhri amesema shambulio hilo ni zaidi ya ukatili wa mafashisti na Manazi, ambapo ameibebesha dhima Marekani kwa kuwezesha uchokozi huo kupitia uungaji mkono wake usioyumba kwa utawala ghasibu wa Israel.

"Mauaji ya leo (jana) na damu za mashahidi wetu zinatoa ujumbe kwa Umma wa Kiislamu na watu wote huru duniani kote: Ni wakati wa kukabiliana na wauaji hawa," amesisitiza.

Hamas: Jinai za Israel Gaza zinashinda uhalifu wa Wanazi

Afisa huyo wa ngazi ya juu wa Hamas ameongeza kuwa: Sambamba na vita vya mauaji ya wavamizi, bado tunashuhudia misimamo dhaifu ya baadhi ya nchi za Kiarabu na Kiislamu.

Wakati huo huo, Mkurugenzi wa huduma za ambulensi huko Gaza amesema vikosi vya Israel vinazuia magari ya kubebea wagonjwa kufika eneo kulikojiri shambulio hilo mjini Rafah, ili kutoa msaada kwa waliojeruhiwa.

Ameongeza kuwa, vituo vya usambazaji wa misaada katika Ukanda wa Gaza vimekuwa vituo vya udhalilishaji, na jumuiya ya kimataifa lazima ivizuie.

342/

Your Comment

You are replying to: .
captcha