Jeshi la Yemen limesema katika taarifa yake leo Jumatatu asubuhi kwamba, kikosi cha makombora cha Wanajeshi wa Yemen kimefanya operesheni maalum ya kijeshi ikilenga uwanja wa ndege wa Ben Gurion katika eneo linalokaliwa kwa mabavu la Yaffa kwa kutumia kombora la balistiki la hypersonic.
Limesema operesheni hiyo imefikia lengo lake kwa mafanikio, na kusababisha mamilioni ya Wazayuni maghasibu kukimbilia kwenye makazi na mahandaki, na kusimamisha shughuli katika angatua hiyo.
Operesheni hiyo ya kupinga Israel ilifanyika leo asubuhi, ambapo vyombo vya habari vya utawala huo vilithibitisha kwamba safari za ndege katika uwanja wa Ben Gurion zilisitishwa baada ya kombora hilo la balistiki la hypersonic kuvurumishwa kutoka Yemen.
Vyombo hivyo pia vimeripoti kuwa, ving’ora vya tahadhari kufuatia shambulizi hilo la anga vilisikika magharibi mwa mji wa al-Quds unaokaliwa kwa mabavu, kutokana na ukubwa na hatari ya kombora hilo la balistiki kutoka Yemen.
Jeshi la Yemen limekuwa lilitekeleza wimbi la mashambulizi dhidi ya ngome za utawala haramu wa Israel na kuusababishia utawala huo hasara kubwa za kijeshi na kiuchumi.
Opereshenei hizo za kishujaa za vikosi vya ulinzi vya Yemen zinafanywa kwa nia ya kuendelea kukabiliana na mauaji ya kimbari ya utawala huo dhidi ya Wapalestina katika Ukanda wa Gaza. Jeshi la Yemen limesisitiza kuwa litaendeleza mashambulizi yake dhidi ya Israel hadi pale utawala huo utakapositisha jinai zake dhidi ya Wapalestina.
342/
Your Comment