"Leo ni Sabato (Jumamosi) hapa. Inapaswa kuwa siku tulivu. Lakini huenda isiwe hivyo. Watu wote wamepewa maagizo ya kukaa karibu na mahandaki," ameandika Mike Huckabee kwenye mtandao wa kijamii wa X.
Operesheni ya kijeshi ya Iran ya kulipiza kisiasi iliyofanyika kwa mafanikio ikiwa na jina la "Ahadi ya Kweli III" ilianza jana Ijumaa na kupiga maeneo kadhaa katika ardhi za Palestina zinazokaliwa kwa mabavu na Wazayuni, ukiwemo mji mkuu, Tel Aviv.
Balozi huyo wa Marekani ni muungaji mkono mkubwa wa utawala wa Kizayuni wa Israel kiasi kwamba hivi karibuni alisema hadharani kuwa, suala la Wapalestina kuwa na nchi yao huru, halina nafasi kwa Marekani.
"Sioni akilini kwamba suala la Palestina kuwa na nchi yao huru linaweza kutokea kwa sababu ya Marekani na Israel ziko karibu sana, zinaaminiana na hilo ndilo neno ninalopenda kulisisitizia - kuna uaminifu kati ya Marekani na Israeli," aliliambia shirika la habari la Israeli Ynet.
Balozi huyo Mayuni alifika mbali na kusema: "Mara nyingi mimi husema, tuna marafiki, tuna washirika, lakini tuna mpenzi mmoja tu, naye ni Israel, na ninaposema hivyo, simaanishi kwamba hatuna uhusiano wa kina na nchi nyingine."
Lakini Mzayuni huyo Mmarekani amelazimika kukiri ukubwa na hasara zilizosababishwa na mashambulizi ya kulipiza kisiasi ya Iran dhidi ya utawala wa Kizayuni akisema kwamba alilazimika kukimbilia kwenye mashimo mara tano wakati wa operesheni hiyo ya Iran.
342/
Your Comment