Kwa mujibu wa Shirika la Habari la Ahlul-Bayt (a.s) -ABNA-, Mashambulio ya makombora ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran dhidi ya utawala wa Kizayuni kwa ajili ya kukabiliana na jinai za utawala ghasibu wa Kizayuni kwa jinai yake ya kulilenga kundi la watu wasio na hatia, makamanda wakuu wa kijeshi na wanasayansi wa nyuklia yamekuwa chemchemi ya kutia moyo na furaha kwa watu wote wanaodhulumiwa duniani. Mbali na uungaji mkono wao mkubwa kwa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran, Umma wa Kiislamu na watu wote wapenda uhuru duniani wanatoa wito wa kuendelezwa mashambulizi hayo hadi kukombolewa kikamilifu Quds Tukufu.
Katika upande mwingine, upuuzi wa Rais wa Marekani na kitisho cha mauaji dhidi ya Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu na mashambulizi katika ardhi ya Iran vimeifanya damu ya mataifa yanayopenda uhuru duniani kuchemka. Mamlaka kuu za kidini, wasomi, wanafikra, na watu wengi katika nchi mbalimbali wameonyesha miitikio iliyoenea kwa ujasiri huo.
Ayatollah Sheikh Hussein Ma'tuq, Mwanachuoni mashuhuri wa Kuwait na mjumbe wa Jumuiya ya Kimataifa ya Ahlul-Bayt (AS) katika mahojiano na Shirika la Habari la ABNA, alivichukulia vita vya hivi sasa kati ya Jamhuri ya Kiislamu na uistikbari wa dunia na adui wa Kizayuni kuwa ni vita vilivyopo baina ya imani na ukafiri, na akasema: Kama vile Mtume wa Mwenyezi Mungu (saww) alivyosema kuhusu Amirul-Muuminin Ali bin Abi Talib (as): "Uislamu wote umesimama dhidi ya ushirikina". Msingi wa vita hivi ni vita vya imani kwa Mwenyezi Mungu na imani katika ahadi ya ushindi wa kimungu dhidi ya dhuluma, ufisadi, batili, kwa sababu hivi ni vita vya uwepo.
Ni wajibu wa Waislamu wote kutetea haki na kusimama upande wa haki, na tuna uhakika kwamba tunakaribia ushindi wa mwisho na tuna uhakika na ahadi ya Mwenyezi Mungu aliposema: -(إِنَّ وَعْدَ اللّهِ حَقٌّ)- "Ahadi ya Mwenyezi Mungu ni ya Haki (ya kweli)". "Wasije wakakufanya wale ambao hawajafikia daraja ya yakini uwe si mwenye msimamo na uwe mwepesi" (Surah Ar-Rum: 60). "Na Mwenyezi Mungu humsaidia anayemnusuru, na Mwenyezi Mungu ni Mwenye nguvu na Hashindwi" (Surah Al-Hajj, 22).
Mwanachuoni huyu mashuhuri wa Kuwait, akizungumzia ulazima wa kukabiliana na maadui wa ukweli na uadilifu, alisema: "Je, huoni kwamba uadilifu hautekelezwi?! Huoni wanachofanya Wazayuni huko Palestina? Je, huoni ufisadi ambao Wazayuni na Marekani wameufanya duniani? Kuvunjiwa heshima Msikiti wa Al-Aqsa kutaendelea hadi lini?" Ni lazima tufanye mapinduzi, tusimame, tusogee mbele, na tuungane chini ya bendera ya Imam Khamenei, Allah (adumishe kivuli chake). Ni lazima tuamini ahadi ya Mwenyezi Mungu aliposema: “Walipowaambia: “Watu (maadui) wamekukusanyieni jeshi (kukupigeni), basi waogopeni,” lakini imani yao ikazidi na wakasema: "Mwenyezi Mungu anatutosha na ni mbora wa wasimamizi" (Sura Al-Imran, 173) na amesema pia: "Shetani ndiye anayewatia khofu marafiki zake, basi msiwaogope bali niogopeni Mimi ikiwa nyinyi ni Waumini" (Sura Al-Imran, 175). Shetani huwaogopesha marafiki zake, hatuogopi Marekani wala mamluki wake.
Amesisitiza kuwa: "Vita na mapambano haya ni mapambano ya Umma wa Kiislamu yaliyoibukia katika nchi Jamhuri ya Kiislamu. Vita hivi havikomei kwenye mipaka ya kijiografia, bali ni vita vya Umma mzima wa Kiislamu dhidi ya ukafiri."
Ayatollah Ma’tuq ameongeza kwa kumalizia mazungumzo yake kwamba: “Tunamuomba Mwenyezi Mungu Mtukufu ushindi wa Waumini na wenye ikhlasi, na tunamuomba atuwekee kivuli cha Imamu Khamenei ili aendelee kutuongoza katika njia hii hadi siku ambayo Israel itatoweka kwenye mandhari ya zama na Mwenyezi Mungu akipenda tuswali katika Msikiti wa Al-Aqsa. Nakumbuka maneno ya wahyi, yaliyosema: “Tumependa kuwaneemesha wanyonge wa ardhi na kuwafanya viongozi na warithi” (Al-Qasas, 5). "Na pia tuliandika katika Zaburi baada ya Taurati kwamba mwishoni waja wangu wema ndio watakaoirithi ardhi" (Al-Anbiya, 105).
Your Comment