22 Juni 2025 - 17:46
Ufafanuzi kuhusu Jibu la Iran kwa Marekani litatekelezwa kwa namna ipi? | Mpango mzima wa Iran ni kuichakaza na kuimaliza Israel - Haina pa kutokea

Iran inasisitiza kuwa vita hii itaendelea hadi utawala wa Kizayuni uangamizwe kabisa, na uingiliaji wowote wa nje utazidisha tu uhamasishaji na ukali wa mapigano ya Iran.

Shirika la Habari la Kimataifa la Ahlul-Bayt (as) -ABNA- Kulingana na vyanzo vya kuaminika, Iran imesisitiza kuwa kuingilia kwa Marekani katika vita hakutaifanya Israeli iweze kuokolewa kutoka kwenye Moto wa Iran, bali pia kutasababisha migogoro yenye matokeo magumu yasiyotarajiwa. 

Kwa mujibu wa ripoti hiyo, Marekani na utawala wa Kizayuni walifikiri kuwa Israel ikisha fanya uchokozi wake dhidi ya Iran, Iran itajibu na vita vitamalizika kwa haraka katika siku za mwanzo, lakini mahesabu hayakuwa namna hiyo, Iran ilichukua hatua ya kuteua uongozi mpya kushika nafasi za Makamanda wa ngazi za juu waliouliwa Kigaidi, kisha ikaanza kuuwasha Moto wa Kisasi dhidi ya Israel kwa  kuishambulia kwa Makombora makubwa, na kuipatia hasara kubwa isiyoweza kufidiwa kirahisi.

Ingawa mauaji ya Makamanda wa Iran yamefanyika kupitia Utawala huu Haram wa Israel, na Mauaji hayo ya kigaidi yamekuwa na athari hasi, lakini hasara zilizotokana na mashambulizi Makali ya Iran dhidi utawala huu zimezidi makisio yao, hawakutarajia walichokutana nacho katika Majibu ya Makombora ya Iran.

Ufafanuzi kuhusu Jibu la Iran kwa Marekani litatekelezwa kwa namna ipi? | Mpango mzima wa Iran ni kuichakaza na ukimaliza Israel - Haina pa kutokea

Iran imejiandaa na inatarajia vita hii itachukua kati ya miezi 2 hadi 6 na imeiweka mipango yake katika mstari ulioonyooka kulingana na hali ya vita ilivyo. Katika picha ni lango bahari la Hormoz ambalo lipo katika meza ya machaguo ya Iran. Iran ikifunga lango bahari muhimu la kiuchumi duniani, Marekani na nchi za Ulaya watajua maana halisi ya kuingia vitani na Iran ni kujitumbukiza katika matatizo makubwa kupindukiwa. Lango hili la Bahari ya Hormoz linapitisha meli nyingi za mafuta na gesi kwenda ulaya na Marekani na sehemu zingine za dunia. Sasa lipo kwenye udhibiti wa Iran na kuna uwezekano mkubwa Iran ikachukua hatua hatua za kulifunga.

Marekani imehamisha vituo vyake; Iran iko makini zaidi

Katika siku za hivi karibuni, kabla ya kuingia rasmi kwa Marekani kwenye vita ili kuisaidia Israel, majeshi yake yalihamisha vituo vyake vya kijeshi katika eneo la kikanda ili kuepuka kutoshambuliwa katika Mashambulizi ya Makombora ya Iran ambapo walikadiria kuwa Iran yaweza kufanya mashambulizi katika vituo hivyo kama sehemu ya majibu yake. Hata hivyo, Iran inasisitiza kuwa haitadanganywa na mbinu hiyo na kuzingatia zaidi ufanisi wa kuangamiza utawala wa Kizayuni ambao ndio msingi mkuu wa Marekani kwenye eneo hili la Mashariki ya Kati.

Kulingana na vyanzo vya kuaminika, Iran ina mpango wa kufanya shambulio la ghafla na la mshangao, huku ikiendelea kuibinya Israeli, na pia ikiendelea kulenga vituo vya Kiuchumi vya Marekani na vya kijeshi katika eneo la kikanda kwa wakati mmoja. 

Muhimu zaidi katika mkakati wa Iran ni kwamba kuingilia kwa Marekani hakipaswi kuzuia utekelezaji wa mipango yake dhidi ya utawala haram wa Kizayuni.

Vita itaendelea hadi Israel itamalizwe na kuangamizwa kabisa

Iran inasisitiza kuwa vita hii itaendelea hadi utawala wa Kizayuni uangamizwe kabisa, na uingiliaji wowote wa nje utazidisha tu uhamasishaji na ukali wa mapigano ya Iran. Wachambuzi wanaona kuwa Iran imejiandaa kwa vita vya muda mrefu kwa kuwa na mpango madhubuti, ikitumia uwezo wake wa kijeshi na kitaarifa kutoa mashambulizi ya mwisho na makali kwa adui.

Tags

Your Comment

You are replying to: .
captcha