Saeed Khatibzadeh, Naibu Waziri wa Mambo ya Nje wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran, katika mahojiano na Al Mayadeen, alitangaza: "Tehran ilisimama imara na kwa nguvu dhidi ya uchokozi wa Israel na ikastahimili. Uchokozi wowote utakaofanywa dhidi ya Iran, tutaujibu kwa nguvu na uthabiti."
Khatibzadeh alifafanua: "Tulishambulia kituo kimoja kilichokuwa chini ya udhibiti wa Amerika. Tuko tayari kujibu uchokozi wowote na Washington ndiyo iliyotutumia ujumbe wa kusitisha vita."
Aliongeza: "Wakazi wa maeneo yanayokaliwa wanapaswa kujua kwamba wao ni waathirika wa makosa ya kimkakati ya Benjamin Netanyahu, Waziri Mkuu wa utawala wa Kizayuni."
Khatibzadeh alisema: "Iran imedhamiria kupinga na utawala wa Kizayuni umepigwa kofi kali."
Naibu Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran aliendelea: "Washington inapaswa kulipa fidia kwa uharibifu iliosababisha kwenye vituo vya Iran, na tutawasilisha malalamiko katika Umoja wa Mataifa."
Saeed Khatibzadeh katika mahojiano na Al Mayadeen alisema: "Huwezi kulipua sayansi na uwezo wa kiufundi na teknolojia nchini Iran."
Alibainisha: "Iran ni ustaarabu na haiwezi kuharibiwa, na Rais wa Amerika anapaswa kujua hili."
Khatibzadeh alisema: "Iran imetangaza waziwazi kuwa uchokozi uliotokea umeharibu kanuni ya diplomasia na Iran haimwamini mpatanishi aliyepanga njama dhidi yetu. Kile ambacho hakikufikiwa kwa uchokozi, hakitafikiwa pia kwa diplomasia."
Alisisitiza: "Rafael Grossi anapaswa kuwajibika baada ya kutekeleza jukumu la kusikitisha kwa kuandaa njia ya makabiliano."
Your Comment