Akizungumza kwa njia ya video kwenye kikao cha mashauriano cha mkutano wa 17 wa kila mwaka wa BRICS mjini Rio de Janeiro jana Jumapili, Putin amesema "Nchi wanachama wa BRICS sio tu wanachangia theluthi moja ya ardhi ya dunia, na karibu nusu ya idadi ya watu wa sayari hii, lakini pia zinachangia asilimia 40 ya uchumi wa dunia."
"Pato la Taifa la pamoja la wanachama wa BRICS linalopimwa kwa uwezo wa kununua tayari linafikia dola trilioni 77 trilioni, hiyo ni kwa mujibu wa data ya Shirika la Fedha Duniani IMF ya 2025," ameongeza hayo na kubainisha kuwa "katika kipimo hiki, BRICS inayapiku kwa kiasi kikubwa baadhi ya makundi mengine, ikiwa ni pamoja na kundi la G7."
Wanachama wa sasa wa kundi la BRICS ni Brazil, Russia, India, China , Afrika Kusini, Misri, Iran, UAE, Saudi Arabia, Indonesia na Ethiopia.
Baadhi ya nchi zinazoendelea kama Algeria, Belarus, Bolovia, Cuna, Indonesia, Kazakhstan, Malaysia, Nigeria, Thailand, Uturuki, Uganda, Uzbekistan na Vietnam zimeeleza nia na hamu yao ya kujiunga na kundi hilo lialoibukia kiuchumi.
Rais wa Russia amebainisha kuwa, nchi wanachama wa BRICS zinazidi kutegemea sarafu zao za kitaifa katika miamala ya kibiashara baina yao. Katika hatua yake ya kuizuia BRICS kuachana na matumizi ya sarafu ya dola, Rais Donald Trump wa Marekani amezitishia nchi wanachama wa kundi hilo dhidi ya hatua yoyote ya kudhoofisha sarafu ya dola.
342/
Your Comment