17 Julai 2025 - 19:01
Israel Yazidisha Mashambulizi ya Anga Kusini mwa Syria

Hadi sasa, Israel haijatoa tamko rasmi kuhusiana na mashambulizi hayo mapya. Shirika la Habari la Ahlul-Bayt (as) litaendelea kufuatilia kwa karibu na kuripoti hali inavyoendelea huko Syria.

Israel Yazidisha Mashambulizi ya Anga Kusini mwa Syria

Shirika la Habari la Kimataifa la Ahlul-Bayt (as) -ABNA- Jana siku ya Jumatano, ndege za kivita za Israel zilifanya mashambulizi makali ya anga katika maeneo mbalimbali ya kusini mwa Syria, zikilenga maeneo nyeti ikiwa ni pamoja na: Makao Makuu ya Kamandi Kuu ya Jeshi la Syria, na eneo la Ikulu ya Rais katikati mwa mji wa Damascus.

Israel Yazidisha Mashambulizi ya Anga Kusini mwa Syria

Kwa mujibu wa mamlaka za afya za Syria, raia mmoja amethibitishwa kufariki dunia huku wengine 18 wakijeruhiwa katika mashambulizi hayo yaliyoathiri mji mkuu wa Damascus.

Ripoti zinaeleza kuwa kulikuwa na angalau mashambulizi matano tofauti ya anga, yote yakiwa yamelenga maeneo ya katikati mwa mji huo mkuu wa Syria.

Video zilizorushwa na televisheni ya kitaifa ya Syria zinaonyesha moshi mzito ukifuka kutoka Uwanja wa Umayyad, ambapo ndipo lilipo jengo la Kamandi Kuu ya Jeshi la Syria.

Hadi sasa, Israel haijatoa tamko rasmi kuhusiana na mashambulizi hayo mapya.

Shirika la Habari la Ahlul-Bayt (as) litaendelea kufuatilia kwa karibu na kuripoti hali inavyoendelea huko Syria.

Your Comment

You are replying to: .
captcha