16 Julai 2025 - 12:46
Taifa Haram la Mazayuni lashambulia vikundi vya Kigaidi vya Al-Julani Katika maeneo ya Mji wa Suwayda, Syria

Vikosi vya Genge la Kigaidi la HTS, vinavyoongozwa na Al-Julani, leo asubuhi viliingia katika Mji wa Suwayda, vikiwa na maagizo yaliyoitwa kuwa Maagizo ya "Kulinda Raia".

Shirika la Habari la Kimataifa la Ahlul-Bayt (as) -ABNA Jeshi la Taifa Haram na Ghasibu la Mazayuni, linaloendelea kuikalia Palestina na Sehemu ya Ardhi za Syria kimabavu, limefanya mashambulizi dhidi ya wapiganaji wa Genge la Kigaidi la HTS (wanaojiita “vikosi vya usalama”) katika jimbo la Suwayda kusini mwa Syria, linaloshikiliwa na kundi la Ahmad al-Julani.

Taifa Haram za Mazayuni lashambulia vikundi vya Kigaidi vya Al-Julani Katika maeneo ya Suwayda, Syria

Viongozi wa Suwayda wakubaliana na HTS kusitisha mapigano. Hii ni baada ya Waziri wa ulinzi wa serikali ya muda ya Syria, Abu Qasr, kutangaza kusitishwa kwa mapigano katika mji wa Suwayda, kusini mwa Syria, baada ya kufikiwa kwa makubaliano na wazee wa kijamii wa Druze.

Vikosi vya Genge la Kigaidi la HTS, ambavyo viliingia mjini asubuhi, vimepewa maagizo ya "kulinda raia". Baada ya oparesheni yao kumalizika, udhibiti wa mji utakabidhiwa kwa vikosi vya usalama wa ndani.

Tags

Your Comment

You are replying to: .
captcha