Kwa mujibu wa shirika la habari la kimataifa la AhlulBayt (AS) – ABNA – likinukuu Al Jazeera, msemaji wa kanda wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Watoto (UNICEF) alionya kwamba Ukanda wa Gaza unakabiliwa na hali mbaya, na eneo hilo limegeuka kuwa makaburi ya watoto kutokana na kutojali kwa ulimwengu.
Aliendelea katika mahojiano na kituo cha Al Jazeera akiongeza: "Mzingiro dhidi ya Ukanda wa Gaza na kuweka vizuizi kwa kuingia kwa misaada ya kibinadamu ndani yake, ndio sababu ya kuongezeka kwa vifo katika eneo hili."
Afisa huyu wa Umoja wa Mataifa alibainisha: "Israeli imekataa maombi mengi ya kuingiza misaada ya kibinadamu Gaza, na kukataa huku kumepelekea kuwepo kwa hali ambayo eneo hili linashuhudia leo."
342/
Your Comment