Kwa mujibu wa shirika la habari la ABNA, akilinukuu kituo cha Al Jazeera cha Qatar, Gideon Saar katika mkutano na Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani Marco Rubio mjini Washington alidai: “Kamwe hakutaundwa serikali inayoitwa Palestina.”
Kwa upande mwingine, Waziri wa Mambo ya Nje wa utawala wa Kizayuni alitangaza kuwa katika mkutano huo, pande mbili, pamoja na kujadili maendeleo ya vita vya Gaza kabla ya mkutano wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa, walijadili suala la Iran na njia za ushirikiano kati ya Washington na Tel Aviv ili kukabiliana na kile kinachodaiwa kuwa “vitisho vya Iran.”
Pia, Saar aliishukuru Marekani kwa misimamo yake ya kuunga mkono utawala wa Kizayuni.
Your Comment