3 Septemba 2025 - 00:19
Source: Parstoday
Barua ya pamoja ya Iran, Russia na China yalitaka Baraza la Usalama lipinge kutekelezwa utaratibu wa Snapback

Mawaziri wa Mambo ya Nje wa Iran, China na Russia wameandika barua ya pamoja wakipinga hatua ya nchi tatu za Ulaya ya kuanzisha "utaratibu wa papo kwa hapo au Snapaback " kwa ajili ya kurejesha vikwazo vya Umoja wa Mataifa dhidi ya Tehran.

Barua hiyo iliyotumwa kwa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa na kwa Mwenyekiti wa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa (UNSC), inatoa wito kwa Baraza hilo kuitambua hatua hiyo ya Ulaya kuwa ni batili. 

Abbas Araqchi Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran ametangaza kuwa ukurasa wake wa mtandao wa kijamii wa X kwamba yeye na Mawaziri wenzake wa Mambo ya Nje wa China na Rusia Wang Yi na Sergei Lavrov wamesaini barua ya pamoja huko Tianjin China ambako wamehudhuria Mkutano wa Jumuiya ya Ushirikiano ya Shanghai (SCO).

Barua hiyo ya pamoja imeandikwa na Iran, Russia na China baada ya Troika ya Ulaya yaani E3 inayoundwa na Uingereza, Ufaransa na Ujerumani nchi ambazo ni wanachama wa makubaliano ya nyuklia ya Iran ya mwaka 2015 ambayo rasmi yanafahamikwa kwa jina la makubaliano ya JCPOA tarehe 28 mwezi Agosti mwaka huu kulitaarifu Baraza la Usalama la UN kwamba wamerejesha utaratibu wa Snapback ambao utapelekea kurejeshwa vikwazo vya Umoja wa Mataifa dhidi ya Iran ambavyo viliondolewa chini ya makubaliano hayo. Nchi hizo tatu zimesema kuwa zimeamua kutangaza kurejesha utaratibu huo wa vikwazo kutokana na kile walichokitaja kuwa "kutofuata sheria Iran."

Inafaa kukumbusha hapa kuwa, Marekani ilijitoa kwa upande mmoja katika makubaliano ya JCPOA  mwaka 2018 wakati wa muhula wa kwanza wa Rais Donald Trump. Mwaka mmoja baadaye, Iran pia ilianza kuchukua hatua mkabala baada ya pande husika za Ulaya katika makubaliano hayo kushinda kufidia hatua ya Marekani ya kujitoa kwa upande mmoja katika makubaliano ya JCPOA. 

Your Comment

You are replying to: .
captcha