15 Septemba 2025 - 23:43
Source: Parstoday
Russia yaionya vikali Ulaya dhidi ya kuchukua mali yake

Serikali ya Russia imezionya vikali nchi za Ulaya kwamba itachukua hatua kali dhidi ya taifa lolote litakalochukua mali yake.

Onyo la Russia limetolewa baada ya baadhi ya ripoti kueleza kwamba Umoja wa Ulaya unapendekeza kutumia mali ya Russia ambayo imezuiwa yenye thamani ya mabilioni ya dola ili kuisaidia Ukraine.

Punde tu baada ya Rais Vladimir Putin wa Russia kupeleka vikosi vyake kuivamia Ukraine mwaka 2022, Marekani na washirika wake walizuia ushirikiano na Benki Kuu ya Russia na vile vile wizara ya Fedha ya Russia. Aidha walizuia mali ya Russia yenye thamani ya kati ya dola bilioni 300 hadi 350. Nyingi ya mali zikiwa ni hati za dhamana za serikali za Ulaya, Marekani na Uingereza zilizohifadhiwa barani Ulaya.

Shirika la habari la Reuters, liliripoti kwamba Rais wa Kamisheni Kuu ya Umoja wa Ulaya Ursula vonder Leyen, anautaka umoja huo kutafuta njia mpya ya kuisadia Ukraine kwa kutumia mali za Russia ambazo zimezuiwa barani Ulaya.

Gazeti la Politico pia liliripoti kuwa Tume ya Ulaya inatafakari wazo la kutumia amana za fedha za russia zilizopo katika Benki Kuu ya Ulaya, zinazotokana na hati za dhamana zinazomilikiwa na Russia, kufadhili ‘mkopo wa fidia' kwa Ukraine.

Wazo hilo limekosolewa vikali na serikali ya Moscow. Rais wa zamani wa Russia Dmitry Medvedev, ambaye kwa sasa anahudumu kama naibu mwenyekiti wa Baraza la Usalama la Russia, ameandika kwenye ukurasa wake wa Telegram kwamba, ikiwa hilo litatimia, Russia itaziandama nchi za Umoja wa Ulaya.

342/

Your Comment

You are replying to: .
captcha