Kwa mujibu wa ripoti ya shirika la habari la ABNA, Wazayuni wanaojulikana kama Waharedi walifanya maandamano dhidi ya kujiunga na jeshi la utawala wa Israel kwa lazima na kufunga barabara namba nne katika eneo la Bnei Brak lililopo katikati ya maeneo yanayokaliwa kwa mabavu.
Vyombo vya habari vya Kiebrania viliripoti kuwa maandamano hayo yalisababisha usumbufu katika harakati za magari kuelekea mji wa Petah Tikva.
Vikosi vya polisi vya utawala wa Kizayuni vilitumwa katika eneo hilo huku vikitangaza kuwa maandamano hayo ni kinyume cha sheria.
Ikumbukwe kuwa mgogoro wa uhaba wa askari katika jeshi la utawala wa Kizayuni umefanya macho yaelekezwe kwenye ulazima wa Waharedi kujiunga na jeshi; suala ambalo limesababisha kuongezeka kwa maandamano miongoni mwao.
Your Comment