6 Januari 2026 - 12:07
Source: ABNA
Urusi: Tunalaani uvamizi wa Marekani nchini Venezuela; Maduro aachiwe huru mara moja

Mwakilishi wa Urusi katika mkutano wa Baraza la Usalama kuhusu Venezuela alisema: "Tunalaani uvamizi wa Marekani huko Caracas ambao ni ukiukaji wa wazi wa sheria za kimataifa, na tunataka kuachiwa huru mara moja kwa Rais mteule na halali wa Venezuela."

Kwa mujibu wa shirika la habari la ABNA kupitia Al Jazeera, Vasily Nebenzia, mwakilishi wa Urusi katika mkutano wa leo Jumatatu wa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa, alisema: "Utawala wa mabavu wa Marekani kwa kutumia nguvu unaathiri makumi ya nchi katika sehemu mbalimbali duniani." Aliongeza: "Tunalaani shambulio la Marekani dhidi ya Venezuela ambalo ni ukiukaji wa wazi wa kanuni zote za sheria za kimataifa. Tunawataka viongozi wa juu wa Marekani kumuachilia mara moja Rais aliyechaguliwa kihalali wa nchi huru pamoja na mkewe." Nebenzia alisisitiza: "Hakuna uhalali wa jinai ya Marekani huko Caracas. Migogoro inapaswa kutatuliwa kwa njia ya mazungumzo."

Your Comment

You are replying to: .
captcha