Shirika la Habari la Kimataifa la Ahlul-Bayt (as) -ABNA- Tatizo la Marekani chini ya Trump dhidi ya Iran halihusiani hasa na Iran kumiliki silaha za nyuklia, bali linahusiana zaidi na uwezo wa Iran wa kuweza kutengeneza silaha hizo.
Kwa maana hiyo, hofu yao si bomu lenyewe, bali ni nguvu, elimu, na uwezo wa Iran wa kuunda bomu la nyuklia kwa kujitegemea. Kinachowaumiza si silaha, bali ni uwezo wa Iran. Ndiyo maana chuki yao imejikita katika kuzuia maendeleo na nguvu za Iran.
Kibri cha dhalimu huyu (Marekani/Trump) hakimaanishi kwamba Mwenyezi Mungu amempuuza au amemsahau. Kinyume chake, kadiri dhalimu anavyozidi kujipandisha juu kwa kibri na majivuno, ndivyo anguko lake linavyozidi kuwa la kutisha zaidi.

Kila muumini anaambiwa: Tulia na umtegemee Mwenyezi Mungu. Adui hataangamia kwa nguvu zetu bali kwa mapenzi ya Allah. Mwenyezi Mungu humchelewesha adui na dhalimu wa Umma, lakini hampuuzi kamwe. Muda wake unapofika, huanguka kutoka pale alipoinuka kwa majivuno, na anguko lake huwa la kishindo kikubwa.
Historia inatufundisha kupitia mifano kama Fir‘aun na Namrud, waliodhani wako juu milele, lakini mwisho wao ulikuwa fedheha na maangamizi.
Your Comment