2 Mei 2026 - 13:18
Source: ABNA
Foreign Policy: Ayatollah Khamenei alikuwa kiongozi wa wanyonge

Vyombo vya habari vya Marekani kwa kurejelea maandamano makubwa duniani kwa kukabiliana na kifo cha kishahidi cha Ayatollah Seyyed Ali Khamenei viliandika: Alikuwa Ayatollah wa wanyonge.

Kwa mujibu wa shirika la habari la ABNA, gazeti la Marekani "Foreign Policy" katika ripoti yake yenye kichwa "Ayatollah wa Wateseka" liliandika: Kwa Waislamu wa mapokeo ya Kisunni wanaoelekea Iran, dhana ya "upinzani" bado inavutia.
Gazeti hili la lugha ya Kiingereza liliandika: Baada ya kuuawa (kifo cha kishahidi) kwa Ayatollah Ali Khamenei, kiongozi wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran, waandamanaji Waoshia huko Karachi, Pakistani na Baghdad, Iraq walivamia ofisi za kidiplomasia za Marekani na kufanya mapigano makali na vikosi vya usalama.
Ingawa hizi zilikuwa athira zenye vurugu zaidi za watu, hazikuwa ndio athira pekee. Duniani kote, watu wengi pia walikusanyika kumuunga mkono Ayatollah huyu. Wiki kadhaa baadaye, maandamano yalitokea katika maeneo kama Kuala Lumpur nchini Malaysia, Jakarta nchini Indonesia, New Delhi nchini India, Kashmir inayodhibitiwa na India, na Istanbul nchini Uturuki.
Foreign Policy iliandika: Uungaji mkono wa Tehran kwa vikundi vya Kioshia kama vile Kata'ib Hezbollah nchini Iraq na Hezbollah nchini Lebanon uko wazi, lakini serikali ya Iran pia imejaribu kupata kibali cha ulimwengu wa Kiislamu na kujionesha kama nguvu inayopambana peke yake dhidi ya utawala wa Magharibi. Katika mchakato huo, imefanikiwa kwa kiasi na kupata uungaji mkono unaovuka mipaka ya kimadhehebu.
Gazeti hili la Marekani liliandika: Iran inaposimama dhidi ya Israeli na Marekani, taswira hii inaimarishwa miongoni mwa Waislamu duniani wanaoamini kuwa kama jumuiya ya kimataifa wana uwezo wa kujilinda. Wafuasi hao wa kimataifa wanamwona Iran kama mwakilishi wao ambaye ameendesha vita ndefu na sasa ameshinda kwa kuilazimisha Marekani na Israeli kusitisha mapigano.

Your Comment

You are replying to: .
captcha