9 Mei 2026 - 13:42
Source: ABNA
The Wall Street Journal: Huenda Mazungumzo kati ya Iran na Marekani yataanza tena

Gazeti la The Wall Street Journal limedai kwamba Tehran na Washington huenda wataanza tena mazungumzo yao ya kwa njia isiyo ya moja kwa moja wiki ijayo katika mji mkuu wa Pakistani.

Kwa mujibu wa shirika la habari la ABNA, gazeti la The Wall Street Journal limedai kwamba Marekani na Iran wanaweza kuanza tena mazungumzo yao ya kwa njia isiyo ya moja kwa moja mapema wiki ijayo huko Islamabad.
Gazeti hilo likitoa taarifa kutoka kwa vyanzo vyenye ufahamu limeandika kwamba pande zote mbili kwa kushirikisha wapatanishi zinatayarisha mkataba wa makubaliano wa vifungu 14 ambao utaweka mfumo wa mazungumzo ya mwezi mmoja ili kumaliza vita.
Kwa mujibu wa ripoti hii, katika waraka huo Iran inaombwa kupunguza ukamataji wa Mlango-Bahari wa Hormuz, na kwa upande mwingine, Marekani pia itaanza hatua kwa hatua kuondoa ukamataji wa bandari za Iran ndani ya siku 30 baada ya kuanza kwa mazungumzo.

Your Comment

You are replying to: .
captcha