9 Mei 2026 - 13:42
Source: ABNA
Vyombo vya habari vya Kizayuni: Kashfa ya hivi karibuni yatetemesha Israel

Vyombo vya habari vya Kizayuni vimeelezea kashfa ya kijasusi katika ardhi iliyokaliwa kwa niaba ya Iran kama "tetemeko la ardhi" la kiusalama katika utawala wa Kizayuni.

Kwa mujibu wa shirika la habari la ABNA, tovuti ya Kizayuni ya I24 News iliripoti kwamba kashfa ya kijasusi kwa ajili ya Iran na kufichuliwa kwa vitendo vya wanajeshi wa Kizayuni kumetetemesha utawala wa Kizayuni.
Katika ripoti hii imeelezwa kwamba wanajeshi hao walihamisha habari nyeti kwa Iran kwa kupokea kiasi cha fedha. Wa-Irani wamefanikiwa kuwaajiri wanajeshi na sio raia wa kawaida tu kama ilivyokuwa zamani.
Hapo awali, shirika la usalama na kijasusi la ndani la utawala wa Kizayuni (Shin Bet) na polisi wa kijeshi wa utawala huo katika taarifa yao ya pamoja walitangaza kufungua kesi ya kijasusi dhidi ya wanajeshi 3 na raia 1.
Katika ripoti hii imeelezwa kwamba washtakiwa walipiga picha za vituo vya treni, vituo vya ununuzi, kamera za usalama na baadhi ya maeneo mengine. Pia wanajeshi 3 waliotajwa wanashitakiwa kwa kutoa picha zinazohusiana na shule ya ufundi ya jeshi la anga la utawala huo kwa upande wa Iran.

Your Comment

You are replying to: .
captcha