Kwa mujibu wa shirika la habari la ABNA, gazeti la Kizayuni la Haaretz liliandika katika makala yake kwamba makampuni mawili ya Israel yamebuni zana za kiteknolojia zinazowezesha kufuatilia watumiaji wa huduma ya intaneti ya satelaiti ya Starlink inayomilikiwa na Elon Musk na kubaini mahali walipo na utambulisho wao. Haaretz linaandika kwamba hatua hii imezua wasiwasi mkubwa kuhusu faragha, ufuatiliaji, na matumizi ya data kwa madhumuni ya kiusalama na kijasusi.
Uchunguzi huu unadai kwamba zana hizi zinauzwa kwa taasisi za kitaifa na za kiusalama za utawala wa Kizayuni pekee kama nyenzo za "kupambana na ugaidi", "kukabiliana na ulanguzi wa dawa za kulevya", "kufuatilia mipaka ya baharini" na "mitandao ya magendo".
Starlink ni moja ya mifumo muhimu zaidi ya intaneti ya satelaiti duniani, inayotegemea zaidi ya satelaiti 8,000 zilizo kwenye mzunguko wa chini wa anga zilizorushwa angani na kampuni ya SpaceX inayomilikiwa na Elon Musk, na hutoa muunganisho wa intaneti katika maeneo ya mbali na yaliyotengwa na miundombinu ya jadi ya mawasiliano.
Katika miaka ya hivi karibuni, huduma hii imekuwa nyenzo muhimu kwa waandamanaji na wapinzani wa kisiasa katika nchi mbalimbali.
Uchunguzi huu unaongeza kwamba moja ya makampuni ni kampuni ya Kizayuni iitwayo "TargeTeam", ambayo inafanya kazi huko Kuprosi, kampuni hii inazalisha mfumo unaoitwa "Stargetz" ambao kwa mujibu wa nyenzo za ndani za uuzaji unaweza kufuatilia takriban vifaa milioni moja vya Starlink katika maeneo mbalimbali duniani.
Kampuni ya Israel "Rayzone" ni kampuni nyingine ya Kizayuni inayotoa uwezo sawa wa kiufundi katika mfumo wa uchambuzi wa data kubwa (big data) sokoni.
Kwa mujibu wa Haaretz, mfumo wa Stargetz unaweza kutambua mahali vilipo vifaa vya mawasiliano ya satelaiti, kufuatilia idadi ya vifaa vilivyounganishwa kwenye kila kituo cha ardhi, na kujaribu kugundua utambulisho wa watumiaji kupitia namba zao za simu za mkononi au akaunti zao zilizounganishwa kwenye mitandao mbalimbali.
Your Comment