Kwa mujibu wa shirika la habari ABNA kwa kunukuu shirika la habari "Shihab", Hazem Qasim alitangaza kwamba msichana mdogo aliuawa Jumanne jioni kufuatia shambulio la ndege za kivita za utawala wa Israel kwenye mahema ya wakimbizi huko Khan Yunis.
Aliongeza kwamba mtoto huyu amejiunga na makumi ya maelfu ya watoto waliopoteza maisha kutokana na mashambulio ya mabomu, njaa, kunyimwa matibabu, na athari za vita.
Msemaji wa Hamas pia, akiukosoa ukimya wa jumuiya ya kimataifa, nchi wanachama wa Umoja wa Nchi za Kiarabu, vyama vya siasa, mabunge, wanachuoni na wasomi wa nchi za Kiarabu, alionya kwamba pande hizi hazijachukua hatua zozote madhubuti kuhusu yanayoendelea Gaza.
Mwishoni, Qasim pia alikosoa utendaji wa Mamlaka ya Palestina na akasema kwamba mamlaka hiyo iliyoko Ramallah imekuwa haijali yanayotokea Gaza.
Your Comment