Kwa mujibu wa Shirika la Habari la Kimataifa la Ahlul-Bayt (as) -ABNA- Waziri wa Mawasiliano na Teknolojia ya Habari wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amekutana na mwenzake wa Iraq mjini Baghdad, ambapo pande hizo mbili zilikubaliana kuimarisha ushirikiano katika sekta ya mawasiliano ili kuboresha huduma zinazotolewa kwa mahujaji wa Arubaini ya Imam Hussein (AS).
Katika mkutano huo, Waziri wa Iran alisisitiza umuhimu wa kuendeleza ushirikiano wa pamoja kati ya Tehran na Baghdad kwa lengo la kuhakikisha ibada na shughuli za Arubaini zinafanyika kwa ufanisi zaidi, huku mahujaji wakipata huduma za mawasiliano zilizo endelevu na zenye ubora wa hali ya juu.
Aidha, alitangaza utayari wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran kushirikisha Iraq uzoefu wake katika nyanja za usalama wa mtandao (cybersecurity), uchumi wa kidijitali na maendeleo ya miundombinu ya mawasiliano, hatua inayolenga kuimarisha uwezo wa sekta hiyo katika nchi hizo mbili.
Maoni yako