Kwa mujibu wa Shirika la Habari la Kimataifa la Ahlul-Bayt (as) –ABNA– Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran, Ismaeil Baqaei, amekosoa vikali madai ya Mkuu wa Sera za Kigeni wa Umoja wa Ulaya, Kaja Kallas, kuhusu hali ya haki za binadamu nchini Iran, akisema kuwa madai hayo yanaonyesha kile alichokiita unafiki mkubwa.
Baqaei ameyasema hayo leo Jumamosi, akijibu kauli za Kallas, ambaye alieleza kile alichokiita wasiwasi wa Umoja wa Ulaya kuhusu hali ya haki za binadamu nchini Iran.
Katika ujumbe wake, Baqaei amehoji namna madai hayo ya Umoja wa Ulaya kuhusu haki za binadamu yanavyoweza kuendana na kutoa msaada wa vifaa na teknolojia kwa mashambulizi ya kijeshi ambayo Iran inayataja kuwa kinyume cha sheria dhidi ya wananchi wake na miundombinu yake.
Amesema Umoja wa Ulaya, kwa upande mwingine, umeshindwa kulaani kile alichokiita uhalifu wa wazi dhidi ya binadamu, au hata kutoa huruma kwa watoto wa Iran waliopoteza maisha na kujeruhiwa vibaya katika mashambulizi hayo.
“Kaja Kallas anazungumzia ‘wasiwasi’ wa Umoja wa Ulaya kuhusu haki za binadamu nchini Iran. Inashangaza kuona namna mtazamo huu wa kudai kutetea haki unavyoweza kuendana na kutoa msaada wa vifaa na kiteknolojia kwa mashambulizi ya kijeshi yasiyo halali dhidi ya wananchi wa Iran na miundombinu yao, huku Umoja wa Ulaya ukishindwa kulaani uhalifu wa wazi dhidi ya binadamu au hata kuonyesha huruma kwa watoto wa Iran waliokatwakatwa miili yao,” Baqaei amesema.
Msemaji huyo wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Iran ameongeza kuwa mwenendo huo hauishii tu katika kupoteza uaminifu, bali unawakilisha, kwa mujibu wa kauli yake, “kuhalalishwa kwa uovu” na kilele cha unafiki.
25 Julai 2026 - 13:46
Msimbo wa Habari: 1844700
Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Iran, Esmaeil Baqaei, amesema madai ya Umoja wa Ulaya kuhusu kuhangaikia haki za binadamu nchini Iran yanakinzana waziwazi na uungaji mkono wake wa vifaa na teknolojia kwa mashambulizi ya kijeshi dhidi ya wananchi na miundombinu ya Iran.
Maoni yako