Mmoja wa waandamanaji hao aliyejitambulisha kwa jina la Bi. Sweet ameiambia televisheni ya Press TV kuwa, ni haki yao kuandamana na ni haki yao kutangaza malalamiko yao hadharani, lakini wanajua pia kuwa kutumia nguvu za polisi kuendeshea nchi ndiyo tabia ya Marekani. Bi Sweet na wenzake wapatao 30 walitiwa mbaroni na maafisa wa polisi wa mjini New York siku ya Ijumaa baada ya kushindwa juhudi za polisi hao za kuzima mwamko wa wananchi wa Marekani wa kupinga ubepari. Maandamano ya kupinga ubepari yameenea kote ulimwenguni na yote yamepata ilhamu ya mapinduzi ya wananchi yaliyoanzia kaskazini mwa Afrika yaani Tunisia na Misri. Waandamanaji wa nchi za Ulaya wanaopinga ubepari wanalalamikia kitendo cha asilimia moja ya watu kudhibiti asilimia 99 ya wananchi wa nchi hizo na wanalalamikia pia kutumiwa utajiri wa nchi zao pamoja na kodi wanazotoa katika masuala ya kuendesha vita nje ya nchi na kuusaidia utawala wa Kizayuni huku asilimia 99 ya wananchi wa nchi hizo wakiteseka kwa ukosefu wa kazi na matatizo mengineyo. Maandamano yameendelea pia katika nchi za Ulaya kama vile Uingereza na Ugiriki.
19 Machi 2011 - 20:30
Msimbo wa Habari: 273859
Abna inatuarifu kuwa:Wananchi wanaoandama nchini Marekani kupinga mfumo wa kibepari wamelalamikia ukandamizaji wanaofanyiwa na watawala wa nchi hiyo wakisema kuwa, Marekani inaendeshwa kidikteta na kipolisi.